Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe  Martine Shigela amekabidhi rasmi vifaa mbalimbali vya kutolea huduma za afya kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Pangani. Vifaa hivi vimeletwa na wazawa wa Pangani, watanzania na wadau mbalimbali wanaoishi Ujerumani, ambapo mratibu wa zoezi hili Ndugu Habib Nuru ameshiriki katika zoezi la kukabidhi vifaa hivi.


 Mhe Shigela amewashkuru wadau hawa wa maendeeo kwa kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya Dr Magufuli na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia jamii yetu. Aidha, amempongeza Mhe Jumaa Aweso kwa kuwashawishi wafadhili hawa kuja kusaidia Pangani na kuhakikisha vifaa hivi vinatoka bandarini na kuja Pangani. 


.Vifaa vilivyo letwa ni pamoja na Advanced Ulta sound (zinazoweza kuangalia mimba iliyo chini ya miezi miwili), Advanced Microscope (zinazoweza kupima saratani), electrocardiogram (kifaa cha kupima moyo), computer na switches, x-ray viewer za vituo vyote vya afya, vitanda vya kisasa na magodoro, vigari vya walemavu na wagonjwa, vifaa vya mazoezi, vifaa vya michezo pamoja na vifaa vya kuhudumia watoto. Vifaa hivi vitasambazwa katika vituo vyetu vya afya vya Mwera na Mkalamo ili kuleta ufanisi katika kutoa huduma za afya. 


 Mhe Shigela amewataka wananchi wa Pangani kupata huduma zote muhimu zinazo patikana katika hospitali ya wilaya badala ya kwenda Bombo kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa. Aidha amewaasa wananchi kuendelea kutumia bima ya afya ya jamii ili kuweza kupata huduma zote za afya kwa gharama nafuu. Amewataka wataalam kuvitunza vifaa hivi ili viweze kutumika sasa na hata baadae.

#PanganiMpya

#KaziIendelee.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...