Charles James, Michuzi TV


SERIKALI imelitaka shirika la Umma la Posta nchini kuhakikisha linashughulikia migogoro mahala pa kazi ili kudhibiti gharama za uendeshajai wa shirika hilo kwa kufuata taratibu, lengo likiwa kuhakikisha kwamba hawazalishi migogoro ili kuleta utulivu sehemu ya kazi.


Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Msajili wa Hazina Athuman Mbuttuka alipokua akifunga mafunzo ya semina elekezi kwa mameneja wa mikoa wa shirika hilo.


Amesema mafunzo hayo yamekuwa na manufaa kwani yameongeza weledi wa namna ya kuyahudumia masoko kutokana na ukuaji wa kasi wa sayansi na teknolojia.


“ Hatuna budi kuwa na kasi katika yale yaliyolengwa kuyafanya huku tukizingatia ubunifu na unyumbulifu, katika kipindi hiki cha mafunzo yenu mligusia kuhusu biashara ya usafirishaji wa sampuli za damu tunaona jinsi shirika linavyoaminiwa na kupewa kazi hii nyeti kwa ustawi wa Nchi yetu kwasababu ya unyeti huu naomba eneo hili lipewe umakini unaostahili ili kuhakikisha kwamba imani ya serikali dhidi ya shirika pamoja na dhamana ya watu ambao imewaamini msiwaangushe," Amesema Mbuttuka.


Aidha amepongeza jitihada zilizofanywa na shirika la Posta nchini ambapo huduma ya usafirishaji kwa njia ya magari umeimarika na kuwezesha usafirishaji wa vifurushi mbalimbali kutoka maeneo yote Nchini. 


Pia ameongeza kuwa mafunzo hayo yakawe chachu ya maarifa na mtaji mzuri kwa viongozi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ikiwa ni Pamoja na kuhakikisha kwamba mafunzo hayo yanafika mpaka ngazi ya chini ya watumishi wengine sehemu zao za kazi.


Mbuttuka amesema kuwa  shirika lipo kwa ajilii ya kutoa huduma kwa jamii hivyo kuna baadhi ya huduma nyeti ambazo shirika la POSTA lazima lizifanye bila kujali kama linapata faida au lah! lakini vilevile ni lazima shirika lijiendeshe kwa kuzingatia ubunifiu wa kuanzisha huduma kwenye maeneo mengine.


Kwa upande wake Postamasta mkuu, Hassan Mwang’ombe amesema kuwa shirika hilo  lipo mbioni kuingia kwenye mfumo wa sayansi na teknolojia (TEHAMA) kwani mpaka sasa mfumo wa EMIS umeshakamilika ambapo huduma mbalimbali tayari zimeingizwa ndani ya kifurushi hicho ikiwa ni Pamoja na kifurushi wa malipo, kifurushi cha EMS Pamoja na huduma ya barua.

 Msajili wa Hazina, Athuman Mbutuka akizungumza wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya semina elekezi za mameneja mikoa wa Shirika la Posta nchini

 Postamasta mkuu Hassan mwang'ombe Akizungumza na wajumbe wa bodi ya POSTA katika hafla ya kufunga mafunzo kwa mameneja wa mikoa wa POSTA mafunzo yaliyofanyika kwa siku tano jijini Dodoma.

Baadhi ya mameneja wa mikoa wa POSTA wakiwa kwenye semina ya kufunga mafunzo ya semina elekezi ya utendaji kwa viongozi jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...