Mkuu wa shule ya Sekondari Victory, Pansiano Mlelwa akizungumza katika mahafali ya 13 ya shule ya Sekondari victory iliyofanyika mwishoni mwa wiki wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Wahitimu wakiimba wakati wa mahafali ya 13 ya shule ya sekondari Victory.
Baadhi ya wahitimu.
Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Pwani, Hildegard Makundi akipokea lisala kutoka kwa wanafunzi wa wanaobaki katika shule ya Sekondari ya Victory katika mahafali ya 13nyaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Bendi ya shule ya sekondari Victory ikitumuiza katika mahafali ya 13 ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
SHULE ya Sekondari Victory iliyopo Mpakani mwa jiji la Dar es Salaam na Mwanzoni mwa Wilaya ya Mkuranga ina mikakati zaidi katika kuhakikisha kuendelea kuboresha zaidi kitaaluma licha ya kuwa inafanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya kidato cha nne.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya 13 ya Kidato cha nne ya Shule ya Sekondari ya Victory tangu kuanzishwa kwake, Mkuu wa shule hiyo, Pansiano Mlelwa amesema kuwa shule hiyo imejizatiti zaidi katika kuwasaidia kwa ukaribu zaidi wanafunzi wenye uwezo wa chini ili kuinua viwango vyao vya ufaulu.

Amesema kuwa ili kuhakikisha wanakuwa vizuri kitaaluma walimu wa shule hiyo wanashirikiana vyema katika kutoa mazoezi ya kutosha kwa wanafunzi na kufanya marudio(Revision) ili kukazia maarifa kwa wanafunzi wote wanaosoma katika shule hiyo.

Licha ya kuwepo na programu mbalimbali shuleni hapa tunawashirikisha kwa ukaribu wanafunzi katika programu za kuchangamsha akili mfano michezo, midahalo....." Amesema Mlelwa.

Hata hivyo shule hiyo imehakikisha kuwa na walimu wa kutosha na wenye sifa wanakuwepo shuleni ili kuwahudumia na kuwasaidia wanafunzi kitaaluma.

Mlelwa amesema kuwa shule ya sekondari Victory inajali hali ya Wazazi au walezi kutokana na kuyumba kiuchumi iliyosababishwa na ugonjwa wa Corona kwa kuwa uchumi wa mtu binafsi na wa Taifa uliyumba hivyo kwa kulitambua hilo shule hiyo ilipunguza ada ya robo ya ada ya pili ya mwaka kwa asilimia 50.

Mlelwa amesema kuwa walifanya hivyo kwa sababu wanajali wazazi na walezi wa watoto wanaosoma shule ya Sekondari Victory na wanajali mahusiano mazuri baina ya shule na wazazi.

Katika kudumisha mahusiano mazuri na wananchi wanaozunguka shule hiyo Mlelwa amesema kuwa shule hiyo inatoa maji bure kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni.

"Hali hii imechangia kutatia changamoto ya maji kwa majirani zetu."Amesema Mlelwa.

Hata hiyo Mlelwa aliwaasa wahitimu kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zinaharibu na kupoeza nguvu kazi ya taifa. 

Hata hivyo wameaswa kumcha Mungu kwani ndio chanzo cha maarifa yote
"Mkumbuke Mungu hasa wakati huu wa ujana wenu mlionao, mkaishi maisha ya sala na dua wakati wote kama ilivyokuwa desturi yenu wakati wote mlipokuwa hapa shuleni na Mungu atawakumbukeni katika shida zenu. Amewaasa Mlelwa.

Kwa mwaka wa masomo 2020 wanafunzi 113 wamehitimu masomo ya Kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Victory kati yao 54 ni wavulana na 59 ni wasichana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...