Baadhi ya wahitimu wakiwa na vyeti walivyotunukiwa katika mahafali ya 20 ya darasa la saba ya shule ya St. Mary's Mbezi juu jijini Dar es Salaam.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
TAASISI ya elimu inayosimamia shule za St. Mary's imepongezwa kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa ngazi za Msingi na Sekondari nchini na hiyo ni pamoja na kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kusongesha mbele gurudumu la elimu.

Akizungumza katika mahafali ya 20 ya darasa la saba yaliyofanyika leo katika shule ya St.Mary's Mbezi juu, jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Elimu vifaa na takwimu Wilaya ya Kinondoni na Afisa michezo wa Manispaa hiyo, Respis Bileha amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ya mfano kwa namna inavyoendesha shughuli za elimu kwa kushirikiana kwa ukaribu na Serikali.

"Bado tunafuata nyendo za Mama Rwakatare, alikua na mawazo mapana sana kuhusu elimu...tulifunga shule kutokana na janga la Corona na zilipofunguliwa mwezi Juni tulielekeza wanafunzi wasifukuzwe kwa kigezo cha ada, na St. Mary's ni moja ya shule zilizowapokea wanafunzi hao na nimesikia mmoja wa wazazi amehaidi kuwa watalipa ada hata kama watoto wao wanamaliza leo, hili ni la kuigwa tutoe huduma kwanza huku wazazi wakitimiza wajibu" ameeleza.

Aidha amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa sekta binafsi na ipo tayari wakati wowote kwa ushirikiano wa kujenga taifa.

Vilevile amezitaka shule Wilayani humo kujenga mazingira ya sanaa na michezo kwa kuwa ni sehemu ya elimu na kwa kufanya hivyo kutawandaa vyema wanafunzi kiakili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hizo Dkt. Rose Rwakatare amesema kuwa watanzania waendeelee kuziamini shule kwa namna zinavyotoa elimu kupitia matokeo na wanafunzi wanaopita katika shule hizo.

"Tumeendelea na tutaendelea kukidhi mahitaji ya elimu kwa watoto wetu na hiyo ni pamoja na kuwaandaa watoto katika kupambana na soko la ajira na hata kuweza kujiajiri wengine" amesema Rose.

Dkt. Rose amesema kuwa mazingira ya ujifunzaji kwa shule hizo ni rafiki na huduma hiyo imefika katika maeneo mbalimbali ikiwemo makao makuu Dodoma, Morogoro na Mbeya.

Pia amewatakia heri wanafunzi hao 116 na wengine kote nchini wanaotarajia kufanya mtihani wao tarehe saba na nane mwezi ujao kuufanya kwa utulivu na nidhamu.
Mkurugenzi wa shule za St.Mary's Dkt.Rose Rwakatare akizungumza wakati wa mahafali ya 20 ya shule hiyo na kusema kuwa wataendelea kumudu 
viwango hivyo kwa kutoa elimu bora zaidi, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Elimu vifaa na takwimu na Afisa Michezo wa Manispaa ya Kinondoni Respis Bileha akizungumza na wanahabari mara baada yakufungwa kwa mahafali ya 20 ya shule hiyo na kusema kuwa Serikali ipo tayari wakati wowote kwa ushirikiano wa kujenga taifa, leo jijini Dar es Salaam.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...