Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV 


WASANII mbalimbali nchini wamepata nafasi ya kushiriki kwenye tamasha kubwa muziki ambalo limepewa jina la Wikiendi ambalo limefanyika katika Viwanja vya Nafasi Art Space Mikocheni jijini Dar es Salaam.


Tamasha hilo limeandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania wakishirikiana na Nafasi Art Space ambapo wasanii mbalimbali wamepata nafasi ya kuonesha uwezo wao katika tasnia hiyo ya muziki wa aina mbalimbali kwa kutoa burudani kwa mashabiki na wapenzi wa wasanii hiyo nchini.


Hata hivyo kabla ya kuanza kwa tamasha hilo waandaji wa tamasha hilo Nafasi Art Space na pamoja na Ubalozi wa Ufaransa nchini walipata nafasi ya kuzungumzia tamasha hilo kubwa ambalo limewakutanisha wasanii na wanamuziki  mbalimbali nchini.


Meneja wa Sanaa za Jukwaani kutoka Nafasi Art Space Kwame Mshauru amesema tamasha hilo kwa kawaida huwa linafanyika kila ifikapo Desemba ya kila mwaka lakini baada ya kujadiliana wameona ni vema likafanyika kipindi hiki.


Hasa kwa kuzingatia  kwa muda mrefu kulikuwa na janga la Corona na hakukua na shughuli zozote, hivyo wameona huu ni wakati muafaka kwa wasanii kukutana  na kutoa burudani kwa mashabiki wao.


"Tunajua  tumepita kipindi kigumu cha Corona, shughuli nyingi zilisimama na hata shughuli za sanaa nazo zilisimama.Leo katika tamasha hili wasanii na wadau wasanaa wanapata fursa ya kushiriki kuendelea kuelimishana kupitia sanaa.


"Tumejaribu  kutafuta njia zilizobora katika kuwakutanisha wasanii,tamasha hili la leo ni kubwa na wasanii watapata nafasi za kuonesha kazi zao za sanaa,"amesema .


Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Masuala ya Utamaduni katika Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Celile Frobertpo amesema kuwa Ufaransa imekuwa ikishirikiana na wasani na wadau wa sanaa katika kuhakikisha sanaa inapewa nafasi.


"Ubalozi wa Ufaransa nchini umekuwa ukishirki kikamilifu katika kuendeleza wasanii na sanaa na mbali ya kushiriki kwenye tamasha hili tumekuwa tukifadhili mafunzo ya sanaa kwa kutumia njia ya mtandao,"amesema.

 

 

 Bendi ya Wanawake (Bahati Band) wakitumbuiza jukwaani katika tamasha la Wikiendi lililofanyika katika viwanja vya Nafasi Art Space Mikocheni jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limeandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa wakishirikiana na Nafasi Art Space

 Meneja wa Sanaa za Jukwaani Kwame Mshauru akizungumza kabla ya kuanza kwa Tamasha la Wikiendi lililofanyika katika viwanja vya Nafasi Art Space Mikocheni jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limeandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa wakishirikiana na Nafasi Art Space

 Head of Development Corporation and Culture Affairs French Embassy, Ms Cecile Frobert akizungumza kabla ya Tamasha la Wikiendi lililofanyika katika viwanja vya Nafasi Art Space Mikocheni jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limeandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa wakishirikiana na Nafasi Art Space

Mkurugenzi wa Bahati Female Band, Irene Themistrocles akizungumza kabla ya kuanza Tamasha la Wikiendi lililofanyika katika viwanja vya Nafasi Art Space Mikocheni jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limeandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa wakishirikiana na Nafasi Art Space

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...