Watu wanalalamika bila ya kuwa na idhibati.


Na Chalila Kibuda,Michuzi TV


SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema  kuwa halina  mgongano wa  kimaslahi ambao  unatokea pale wanapotekeleza majukumu yao. 

 

Shirika  hilo limesema hayo kutokana na watu wanatengeneza taarifa juu utoaji huduma kuwa na mapungufu ,wakati uwepo wa shirika ni  kwa mujibu wa sheria na utendaji wake hauingiliani na taasisi zingine katika utoaji huduma na hawashindani ma mtu yeyote.


Akizungumza jijini  Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Emmanuel Ndomba amesema  shirika hilo limekuwa likikejeliwa kutotekeleza kazi zake kiuweledi huku wengi wakienda mbali zaidi wakilishutumiu shirika hilo kuwa  halina watendaji wenye uweledi.


Ndomba amesema kuwa watu wanalalamika lakini hawana idhibati ya kile wanacholalamika nacho na Taasisi ikilalamikiwa ni kunahitaji kutoa ufafanuzi.


“Kuna nia ovu inayoenezwa kuwa TASAC haina wataalamu wenye ujuzi wakati  wataalamu wenye uweledi 306 walioajiriwa na wengine  zaidi ya 120 wa muda mfupi  na tayari tumesajili meli 375 katika kipindi kifupi cha utendaji wetu  huu ni mwaka mmoja tu tangu tuanze kazi haya ni maendeleo makubwa”alisema.


Ndomba amesema mbali na uvumi huo kumekuwa na taarifa kuwa TASAC haiingii mikataba na wnye meli hivyo utendaji wake si wenye kuzingatia uweledi.

 

“Meli zinapokuja ambazo haziko katika safari za mara kwa mara  hapa nchini maana yake tumeshapokea barua pepe kutoka  kampuni husika hivyo hakuna haja ya  kuingia mikataba tena hiyo ni mifumo ya zamani lazima tufanye kazi kulingana na mabadiliko ya teknolojia”alisema.


Ndomba amesema watu wanaovumisha taarifa hizo wanalengo la kuichafua TASAC huku akisisitiza kuwa hakuna muingiliano wa majukumu yeyote wa kiunedeji baina ya shirika hilo na taasisi binafsi.


Pia wanavumisha kwamba gharama   tunazotoza kwa kontena linaloingia baharini ni kubwa,wameenda mbali zaidi kutusukuma kuanza kutoza ambapo meli zitatozwa  sh 2  wakati huduma hiyo awali ilikuwa wanatozwa kutoka Dola nane hadi 14.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC) Emmanuel Ndomba akizungumza na waandishi habari kuhusiana na malalamiko dhidi yao katika utoaji huduma ,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...