Na.Samwel Mtuwa - Geita.


Timu ya Wataalam mbalimbali  wa Jiolojia kutoka  Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wa GST Dkt . Mussa Budeba yatua mkoani Geita kwa ajili ya kutoa Elimu kwa wadau wa sekta ya Madini  katika maonesho ya Tatu ya Tekinolojia na Uwekezaji kwenye sekta ya Madini yanayoanza Leo Septemba 17, 2020.


Sambamba na maonesho haya siku ya Septemba 18 ,2020 kuanzia saa 4:00-5:00 GST itawasilisha mada maalumu juu ya Mbinu za kisasa za  Utafutaji Madini.


 Pamoja na mada hiyo katika Banda la GST pia itatoa Elimu kupitia vifaa vyake , machapisho ya Utafiti wa jiosayansi , Ramani za Utafiti wa Jiosayansi.


Maonesho haya ya tatu yamebebwa na kauli mbiu inayosema "Madini ni Uchumi 2020, Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Taifa"  yanatarajiwa kufunguliwa rasmi septemba 21 , 2020 na  kufungwa septemba 27 ,2020 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania  .


Pichani Mwenyekiti  wa Tume ya Madini Profesa Idriss kikula  akiambatana na Terence Ngole Kamishna Msaidizi wa masuala ya ushirikishwaji wa wachimbaji wadogo (Local Content) kutoka Tume ya Madini wakijadiliana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala GST Omary Mbwana wakiwa katika Banda la GST  Picha zingine ni Muonekano wa Banda la GST pamoja na Wataalam wa GST wakiwa katika Banda.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...