*Baada ya miaka 30 wananchi kuona huduma hiyo 


Na Chalila Kibuda,Michuzi TV.


Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuanza Safari za Train kwa kuanzia Arusha -Dar  es Salaam kuanzia Oktoba 2 mwaka huu.


Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Mhandisi Masanja Kadogosa  amesema kuanza kwa Safari hizo ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuwarahisishia usafiri wa gharama nafuu.


Amesema kuwa usafiri ulikuwepo miaka 30 iliyopita lakini kutokana na mikakati ya serikali ya awamu ya Tano wameweza kurejesha huduma hiyo kwa wananchi.


Amesema kuwa katika Safari zitakazoanza zitakuwa na punguzo kwa asilimia 15 kwa kipindi cha mwezi mmoja.


Aidha amesema kuwa huduma ya train ya mizigo inaendelea na kusaidia katika usafirisha wa bidhaa mbalimbali katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na wafanyabiashara wameishukuru kurudisha train hiyo.


Amesema huduma za usafiri zitakuwa ni endelevu ikiwa ni pamoja watalii kutumia huduma hiyo katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kurejesha huduma za usafiri wa Train kutoka Arusha-Dar es Salaam utakaoanza Oktoba 2 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...