Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Itigi

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) amesema wakati huu wa kampeni kuna mengi yanazungumzwa na kwamba kuna wagombea wengine wanataka kuigawa Tanzania vipande vipande.

Dk.Magufuli amesema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Itigi wilayani Manyoni mkoani Singida na kwamba ameshangazwa sana na hao wanaotaka kuigawa nchi vipande kwa mfumo wa majimbo.

"Nchi hii imejengwa kwa nguvu kubwa ya baba wa Taifa, muanzilishi wa Taifa hili aliyehangaika na wazee wengine wa taifa hili na wengine wako hapa hadi tukapata uhuru, tulikopata uhuru tukawekwa wote kama taifa moja, dini zote , makabila yote tukawa wamoja.

"Hili ni taifa la Tanzania na tukaaungana na wenzetu wa Zanzibar ikazaliwa Tanzania.Umoja ni nguvu, unapomsikia mtu anasimama hadharani bila hata kumuogopa Mungu kwamba akipata madaraka anaigawanyagawanya vipande Tanzania iwe majimbo sio sawa hata kidogo.

"Ndugu zangu hawa muwafundishe kwa kuwanyima kura siku ya Oktoba 28 kwani wanaokotupeleka sio huko , nawatolea mfano tumejenga barabara kutoka Itigi kwenda Chaya kilometa 89 tulitumia Sh.bilioni 103 ,tumejenga barabara ya kutoka Chaya hadi Nyahua kilometa 85 ambapo Sh.bilioni 117zimetumika. Ukijumlisha zote unapata zadi ya Sh.bilioni 200 na kitu zitumika bado hujaweka na vituo vya afya, hujaweka umeme , bado hujaweka na elimu tunayotoa bure kwa watoto wa Watanzania wote, sasa tukigawanya maeneo kwa ajimbo hii barabara Itigi mngeijenga?

"Mnapotengeneza majimbo ya kiutawala , maana yake mtawala wa pale lazima awe wa kabila la hapo.Utakapoweka majimbo utachagua kabila gani litawale pale"Lakini hebu tuangalie sisi tunapotaka kujenga barabara kwa mfano hii fedha tumetoa za Watanzania wote,"amesema Dk.Magufuli.

Amefafanua kuwa hao wenye sera za kuigawa nchi kwa majimbo wanataka kuirudisha nyuma Tanzania na wanataka kuleta mambo ya ukabila na majimbo."Naomba mkatae, ukabila na umajimbo umepitwa na wakati.

"Ukishatenga hivyo maana yake majimbo masikini yatakuwa masikini wa kutupa, kwasababu kwenye majimbo mengine labda kutakuwa na machimbo ya dhahabu ,mengine yana mbuga za wanyama , watalii wanakuja wanaleta dola,kuna jimbo lingine ambalo la Dar es salaam wana TRA iko pale, wana bandari wana mali huku wengine wa Itigi twafaa,"amesema Dk.Magufuli.

Hivyo amewataka wananchi hao kuwatakaa wanaotaka kuleta masuala ya majimbo yanayotaka kuyaleta na kwamba wakoloni walivyotaka kuitawala dunia waligawa kwenye majimbo hivyo, wakatengeneza nchi , wakatengeneza mipaka.

"Sasa kama wamefundishwa hawa waliokuwa na sera ya kutaka kutugawa kataeni, njia ya kukataa ni oktoba 28 asubuhi, tukafagie nje wajifunze, Tanzania sio ya kufanyiwa majaribio,"amesema Dk.Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...