Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika akizungumza kuhusu namna wanavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania, Umoja wa Mataifa na washirika wa maendeleo kwa mchango na ushiriki wao ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu wakati wa uzinduzi wa ripoti inayoonyesha namna lilivyowekeza katika miradi ya maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Zlatan Milisic .
 Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Zlatan Milisic akizungumza kuhusu Umoja wa Mataifa (UN) unashirikiana na serikali ili kufikia vipaumbele vyake pamoja na malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) wakati wa uzinduzi wa ripoti inayoonyesha namna lilivyowekeza katika miradi ya maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. 
Mkutano ukiendelea wakati wa uzinduzi wa ripoti inayoonyesha namna lilivyowekeza katika miradi ya maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania .
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Zlatan Milisic(kushoto) pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika(kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti inayoonyesha namna ilivyowekeza katika miradi ya maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika akizungumza namna walivyojipanga kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali mara baada ya kuzindua ripoti inayoonyesha namna lilivyowekeza katika miradi ya maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Zlatan Milisic
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania,  Zlatan Milisic akitoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa mitaji ya Maendeleo (UNCDF) lilivyoweza kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Tanzania mara baada ya kuzindua ripoti inayoonyesha namna lilivyowekeza katika miradi ya maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Kulia ni Mkuu wa UNCDF nchini Tanzania, Peter Malika
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini Tanzania,Peter Malika akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya wakati wa uzinduzi wa ripoti inayoonyesha namna lilivyowekeza katika miradi ya maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa mitaji ya Maendeleo (UNCDF), limezindua ripoti inayoonyesha namna lilivyowekeza katika miradi ya maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Shirika hilo limesaidia kufanikisha utekelezaji wa miradi yenye thamani zaidi ya dola za kimarekani, milioni 50.6 katika sekta za nishati endelevu, uwezeshaji wa wanawake na vijana kiuchumi, uboreshaji wa mnyororo wa thamani kwenye kilimo, kuhimili mabadiliko ya tabia nchi na miundombinu ya utoaji huduma za kijamii.

Aidha, ripoti hiyo imesheheni taarifa za kina juu ya mafunzo na mafanikio ambayo walengwa na wadau wa UNCDF wameweza kunufaika kupitia programu ya Mpango wa uwezeshaji wa fedha za ndani[Local Finance Initiative] (LFI) kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 kwa kushirikiana na wizara na taasisi za serikali, washirika wa maendeleo, mamlaka za serikali za mitaa na sekta binafsi katika kutatua changamoto kubwa za maendeleo zinazozikumba nchi zinazoendelea.

Mafanikio ya Tanzania kuingia kwenye orodha ya nchi zenye uchumi wa kati yamechochea mijadala kuhusiana na maendeleo endelevu na ukuaji jumuishi. Ripoti hiyo imedokeza mbinu zilizotumika katika kuchangia kuleta mabadiliko ya uchumi wa ndani kwenye nchi washirika ikiwa ni sehemu mahususi ya maendeleo endelevu. Hivyo, uzoefu wa UNCDF unatazamwa kama chombo cha maarifa’ kwa ajili ya mabadiliko ya uwekezaji wa ndani na utekelezaji wa mbinu suluhishi za maendeleo.

Tukio hilo liliwaleta pamoja maafisa wakuu serikali na Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa na kutoa fursa ya kipekee kwa washirika, wadau, na vyombo vya habari kusikia juu ya juhudi za UNCDF katika kutekeleza programu zake zilizolenga kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu (SDG) yanafikiwa nchini Tanzania pamoja na mataifa mengine yanayoendelea.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Bw. Zlatan Milisic aliongeza kuwa, Umoja wa Mataifa (UN) unashirikiana na serikali ili kufikia vipaumbele vyake pamoja na malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

Naye Mkuu wa UNCDF nchini Tanzania, Bwana Peter Malika, aliishukuru serikali, Umoja wa Mataifa na washirika wa maendeleo kwa mchango na ushiriki wao ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu. “Ili kukabiliana na changamoto za wakati huu, tunafanya kazi na taasisisi za umma na sekta binafsi kujenga mnyororo wa thamani ambao utachangia katika  kutengeneza ajira, ujasiriamali na fursa za kibiashara jambo ambalo litaleta mabadiliko chanya ya kiuchumi na kijamii”. Aidha, Bwana Malika alisisitiza kuwa jitihada za kuendeleza uchumi zinapaswa kuzingatia matumizi ya rasilimali yenye tija na uwezo wa kitaasisi katika kuleta mabadiliko ya uchumi jumuishi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...