Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
UONGOZI thabiti na usimamizi wa Shule zinazoongoza na Mutembei Holding Limited watajwa kuwa ndio chachu ya matokeo mazuri kitaaluma katika shule ya sekondari Victory.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa shule ya Sekondari Victory, Ponsiano Mlelwa akizungumza wakati wa mahafali ya 13 katika shule ya Sekondari ya Victory iliyopo mpakani mwa wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani na jijini la Dar es Salaam.

Amesema kuwa shule zinazoongozwa na Mtembei Holding Limited zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma kwa miaka mitatu mfululizo kwa matokeo ya kidato cha pili na kidato cha nne.

"Kwa mwaka 2017 wanafunzi 179 walifanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne ambapo wanafunzi 178 walifaulu na ufaulu huo ni asilimia 99.4, kwa mwaka 2018 wanafunzi 155 walifanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne ambapo wanafunzi 154 walifaulu na ufaulu huo ni sawa na asilimia 99.4 pia na kwa mwaka 2019 wanafunzi 152 walifanya mtihani wataifa wa kidato cha nne ambapo wanafunzi wote walifaulu na ufaulu huo ni sawa na asilimia 100." Amesema Mlelwa.

Hata hivyo amesema kuwa Kumcha mwenyezi Mungu ni chanzo cha maarifa na hekima zote hiyo ndio mbinu kuu inayowafikisha katika viwango vya juu katika ufaulu mwa mitihani katika shule ya sekondari ya Victory.

Mlelwa amesema kuwa shule ya sekondari ya Victory inajivunia kuwa na madarasa ya kutosheleza mahitaji yote ya wanafunzi, wanamaabara tatu za kisasa za masomo ya Biolojia, Kemia ba Fiziki pamoja na Kompyuta ambazo zinawasaidia wanafunzi kusoma.

Hata hivyo Mlelwa amesema kuwa ujenzi wa maabara za masomo ya Sayansi ni juhudi za Mkurugenzi wa shule hiyo kuunga mkono mpango wa serikali unaosisitiza na kuhimiza ujenzi wa maabara kwa kila shule kama ishara ya kuwahamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo.

"Maono ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya Viwanda yapate kutimia katika Ukamilifu wake."Amesema Mlelwa.

Motisha zinazotolewa na Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Victory ndio zinachochea walimu wanaofanya vizuri katika masomo wanayofundisha na kuongeza ufaulu katika shule hiyo.

Amesema kuwa walimu wa shule hiyo wamekuwa wakijitoa na kujituma kuwasaidia vijana wanaosoma shule ya victory mchana na usiku ili kuwaandaa kuhakikisha wote wanafanya vizuri katika mtihani yao ya ndani na ya Kitaifa.

Licha ya hayo Mlelwa amesema kuwa shule ya Sekondari Victory imejizatiti kutoa huduma bora za maji safi na salama, huduma za afya, Chakula, umeme pamoja na Ulinzi kwa wanafunzi wote katika vipindi vyote wanapokuwepo shuleni.

Amesema kuwa mazingira ya shule hiyo ni rafiki kwa wanfunzi kujifunza pasi na shaka yeyote na hivyo kuongeza kiwango cha Ufaulu.

Hata hivyo shule ya Sekondari Victory ni shule mojawapo inayomilikiwa na Mtembei Holdingi Limited(MHL)ambapo shule nyingine zinazomilikiwa na MHL ni shule ya St. Methew's, Ujenzi Mkuranga St. Mark's pamoja na Image Vosa iliyopo Mkoani Iringa.
Viongozi Mbalimbali wa shule ya sekondari ya Victory wakiwa katika maafali ya 13 ya shule hiyo yaliyofanyika.
Wahitimu wakiurudika.
Burudani ikiendelea katika mahafali ya 13 ya shule ya sekondari Victory.


Washindi wa mchezo wa kufukuza kuku wakifurahia kumkamata kuku katika mahafali ya shule ya Sekondari Victory.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...