Na Erick Mwanakulya, Mbeya
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff ameagiza usanifu wa miradi yote ya barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami chini ya mradi wa Agri-Connect kupitiwa upya ili kurekebisha kasoro katika maeneo ambayo yana shida ili ziweze kuwa zenye viwango na ubora kwa mahitaji ya sasa.

 

Mtendaji Mkuu aliyasema hayo jijini Mbeya alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo inayofadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) na kusimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

“Tulikuwa na tatizo la usanifu katika miradi yote ya Agri-Connect lakini sasa usanifu unapitiwa ili kurekebisha maeneo yote yenye shida”, alisema Mhandisi Seff.

Mtendaji Mkuu amesema kuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe jumla ya km 11 zinajengwa kwa kiwango cha lami na tayari ameshamuelekeza Mkandarasi GS Contractors anayetekeleza ujenzi wa Barabara ya Masebe DSP – Mpuguso TCC – Bugoba Kibaoni yenye urefu wa Km 4.9, na Mkandarasi Summer Construction Ltd anayetekeleza ujenzi wa Barabara ya Masebe – Lugoba – Lutete yenye urefu wa Km 7.2 kuhakikisha wanamaliza miradi hiyo ifikapo mwezi Desemba, 2020 kulingana na mkataba.

“Nimepita katika miradi inayotekelezwa na nimewaelekeza wafanye kazi kwa viwango, pia wamenihaidi kufikia mwezi Desemba 2020 watakuwa wamemaliza miradi hii kama muda ulivyopangwa japokuwa wapo nyuma ya muda, pia kutoka barabara kuu barabara yetu inaanzia katikati kipande kingine kinatekelezwa na TANROADS nimewaelekeza wafanye usanifu sehemu ya kipande cha mita 800 ili kuwe na muendelezo wa lami kutoka barabara kuu”.

Aidha, Mhandisi Seff alionesha kutoridhishwa na kasi ya Mkandarasi M/S Canopies International Ltd anayetekeleza Barabara ya Lupeta – Wimba – Zumbwe yenye urefu wa Km 10.1km na Mkandarasi Milembe Construction anayetekeleza Barabara ya Inyala – Simambwe yenye urefu wa Km 16.7 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya vijijini kutokana na kasi ya utekelezaji kuwa chini na hivyo watashindwa kumaliza miradi hiyo kwa wakati.

“Maendeleo ya miradi hayaridhishi, hivyo nimemwacha mwandisi kutoka Makao Makuu ili ashirikiane na wahandisi wa hapa Mbeya vijijini kupitia upya miradi yote na kuja mapendekezo na jinsi ya kutatua changamoto ambazo zimejitokeza katika miradi hii”, alisema Mtendaji Mkuu wa TARURA.

Ameongeza kuwa Wakandarasi ni kama hawafahamu ukubwa wa kazi waliyonayo kwa maana muda umepita kwa asilimia 50 na utekelezaji wa kazi upo chini ya asilimia 20 kitu ambacho kinaonyesha kwa miezi minne iliyobaki hawawezi kumaliza miradi hiyo kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Mtendaji Mkuu amemuelekeza Mratibu wa TARURA Mkoa wa Mbeya pamoja na Mameneja wa TARURA katika Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanasimamia miradi iliyopo katika maeneo yao ya kazi. Vile vile, amemtaka Meneja wa TARURA katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha anafanya ukarabati wa barabara kwenye eneo lake kwakuwa hali yake hairidhishi.

Miradi ya Agri-Connect ina lengo la kuwawezesha wakulima kusafirisha mazao yao kwa urahisi kutoka mashambani kwenda sokoni ikiwa inagusa mazao mbali mbali yakiwemo chai, kahawa, mbogamboga na matunda ambayo inatekelezwa katika Mkoa wa Iringa (Kilolo DC na Mufindi DC) pamoja na Mbeya (Mbeya DC na Rungwe DC).

jenzi wa Barabara ya Inyala–Simambwe kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km 16.7 ukiwa unaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, mkoani Mbeya. Barabara hii inajengwa chini ya mradi wa Agri-Connect inayofadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), na kusimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff (mwenye fulana ya bluu), akitoa maelekezo kwa Wahandisi wa TARURA pamoja na Mkandarasi Milembe Construction wakati akikagua ujenzi wa Barabara ya Inyala–Simambwe kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km 16.7 iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, mkoani Mbeya.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff (mwenye fulana ya bluu), akikagua ujenzi wa Barabara ya Lupeta–Wimba–Zumbwe kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km 10.1 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, mkoani Mbeya. Barabara hii inajengwa chini ya mradi wa Agri-Connect unaofadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), na kusimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Ujenzi wa Barabara ya Masebe DSP–Mpuguso TCC–Bugoba Kibaoni kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km 4.9 ukiwa unaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Barabara hii inajengwa chini ya mradi wa Agri-Connect unaofadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), na kusimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...