Umoja wa Miradi kwa Viziwi Tanzania (Umivita) umeishukuru sana taasisi ya Wakala wa Vipimo kwa kutoa elimu ya Vipimo kwa Viziwi wakati wa maadhimisho ya wiki ya Viziwi kitaifa Mkoani Tabora. Wamesema kuwa kwa muda mrefu makundi ya watu wenye ulemavu yamekuwa yakisahaulika kupata elimu mbalimbali hususani elimu ya vipimo ambayo inaumuhimu sana katika maisha ya kila siku ya Mwananchi kwa kuwa huwezi tenganisha matumizi ya vipimo katika maisha ya kila siku ya mwanadamu na wameomba elimu hiyo iliyotolewa kuhusu vipimo iwe endelevu kwani watu wengi wameifurahia na kuielewa sana.

Akizungumza wakati wa uwasilishaji mada Bw. Anyitike Tumaini ambaye ni Afisa Vipimo amewaeleza kuwa Wakala wa Vipimo ni Taasisi ya Serikali inayosimamia Vipimo vyote nchini kwa mujibu wa Sheria ili kuhakikisha kwamba vipimo hivyo vinapima kwa usahihi na bidhaa zinazouzwa ziko sahihi. Lengo kuu la kusimamia usahihi wa vipimo ni kumlinda mlaji asipunjwe kutokana na vipimo na kuhakikisha anapata bidhaa kwa usahihi kulingana na thamani ya pesa yake.

   Bw. Anyitike Tumaini pia, amewaeleza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura Na. 340 na mapitio yake mbalimbali Wakala inatekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika kwenye Biashara na huduma mbalimbali kama vile Afya, Usalama na Mazingira; Kuilinda jamii dhidi ya madhara yatokanayo na matokeo ya upimaji usio sahihi; Kuhifadhi usahihi wa vipimo toka Vipimo vyenye usahihi wa chini hadi vyenye usahihi wa ngazi ya kati; Kusimamia matumizi sahihi ya vipimo kwa njia ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara; Kukagua bidhaa zilizofungashwa toka nje ya nchi na zile zinazozalishwa hapa nchini; Kuidhinisha aina mpya ya vipimo  vinavyoagizwa toka nje ya nchi na vinavyoundwa hapa nchini; Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na vipimo; Kutoa vibali vya Ugezi na leseni za ufundi na uundaji wa vipimo mbalimbali; pamoja na Kuiwakilisha nchi Kikanda na Kimataifa katika masuala ya vipimo.

Katika maadhimisho hayo ya wiki ya Viziwi Kimataifa wajumbe wameelezwa kuwa Wakala wa Vipimo ina mchango mkubwa katika sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa Serikali inakusanya mapato kwa usahihi kwani Mamlaka ya Mapato nchini hutumia kigezo cha vipimo mbalimbali wakati inapotoza kodi kwa bidhaa mbalimbali. (Mfano: uzito; tani au kilogramu, ujazo: lita, urefu: mita, n.k.). Vile vile vipimo husaidia katika kulinda miundombinu na Usafirishaji ambapo Vyombo vya usafiri hubeba bidhaa/mizigo au abiria kulingana na uwezo (carrying capacity), hivyo kuepusha ajali na uharibifu wa miundombinu kama barabara na reli nakupunguza matukio ya ajali.

Katika sekta ya Kilimo Mkulima hutumia vipimo vilivyo sahihi katika matumizi ya pembejeo wakati wa uzalishaji na wakati wa kuuza Mazao yake ili apate thamani kulingana na gharama alizotumia na uhakiki wa mizani zote zinazotumikia kuuzia mazao mbalimbali hufanyika ili kuhakikisha wakulima hawapunjiki wanauza bidhaa zao katika mizani sahihi. Pia katika sekta ya Viwanda Wakala hufanya uhakiki wa bidhaa zinazotengenezwa viwandani hutegemea vipimo ambavyo hutumika kupimia malighafi na mahitaji mengine. Pia bidhaa zilizozalishwa bado hutegemea usahihi wa vipimo wakati wa kufungashwa katika ujazo, urefu au uzito tayari kwa kusambazwa katika masoko.

Wakala wa Vipimo hufanya uhakiki katika vipimo mbalimbali ili kuhakikisha vinapima kwa usahihi na kaguzi za kushtukiza pia hufanyika mara kwa mara ili kujiridhisha kama vipimo vinatumika kwa usahihi. Mara baada ya uhakiki wa vipimo kufanyika alama mbalimbali huwekwa ili kutambulisha kipimo kilichohakikiwa ambapo alama ziwekwazo ni pamoja na kufunga lakiri (seal) pamoja na stika maalum ya Wakala wa Vipimo.

Meneja wa Wakala wa Vipimo Tabora Bw. Mrisho Mandari amewataka washiriki wa maadhimisho hayo kutojihusisha na matumizi ya Vipimo batili kama ndoo, makopo, na visado kwani kufanya hivyo ni kinyume na Sheria ya Wakala wa Vipimo na kanuni zake. Vipimo batili vinahasara kubwa ambapo mara nyingi huwapunja wafanyabiashara kwa kuuza bidhaa nyingi tofauti na ambavyo wangetumia mizani wangeweza kuuza bidhaa kwa wingi na kwa kujipatia kipato zaidi kulingana na bidhaa wanazouza. Pia, vipimo batili huikosesha serikali kutokusanya mapata kwa usahihi kama inavyo stahili.

Kadhalika,  Bw. Mandari ametoa rai kwa wafanyabiashara kutojihusisha na vitendo vya uchezeaji mizani kwani kufanya hivyo ni kinyume na Sheria ya Vipimo Sura na 340 na mapitio yake mbalimbali ambapo mtu yeyote atakaye kamatwa akichezea vipimo adhabu yake ni faini isiyopungua laki moja (100,000/=) na isiyozidi Millioni ishirini (20,000,000/=) kwa kila kosa. Vile vile amesema kuwa Ofisi za Wakala wa Vipimo zinapatikana katika mikoa yote Tanzania Bara hivyo emdapo mtu yeyote atapata changamoto ya kivipimo au kuitaji ushauri asisite kufika katika ofisi zetu kwa usaidizi wa karibu. Kwa kumalIzia Meneja Mandari amewaeleza kuwa Wakala wa Vipimo imeanzisha namba maalumu ya bure kabisa kwa ajili ya kupokelea maoni na malalamiko ya Wananchi hivyo wasisite kutoa taarifa mbalimbali zitakazo saidia kuboresha utendaji wa Majukumu yetu na namba hiyo ni 0800 11 00 97.

Afisa Vipimo Mkoa wa Tabora Bw. Tumaini Anyitike akitoa elimu ya Vipimo katika maadhimisho ya siku ya viziwi Kimataifa

Washiriki wa Mkutano wakifuatilia elimu ya Vipimo

Afisa wa Wakala wa Vipimo Bi. Rehema Michael akieleza umuhimu wa Wakala wa Vipimo kufanya uhakiki wa bidhaa zinazofungashwa viwandani mfano; maji ya kunywa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...