MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu wanne waliomuua Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk.Sengondo Mvungi baada ya kutiwa hatiani.


Aidha mahakama imemuachia huru mshtakiwa Juma Kanungu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha mashaka dhidi yake.


Hukumu hiyo imesomwa Septemba 17, 2020 na Jaji Kulita Seif Kulita ikiwa ni miaka takribani 7 tangu watu hao wafikishwe kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 22, 2013 na kusomewa kesi ya mauaji.


Waliohukumiwa kifungo ni Msigwa Matonya, Mianda Mlelwa, maarufu kama white,  Paul Mdonondo, Longishu Losingo na John Mayunga maarufu kama Ngosha .


Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kulita amesema, upande wa mashtaka kupitia mashahidi 16 waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi na vielelezo 15 wameweza kuthibitisha pasipo na shaka kuwa watuhumiwa hao watano wametenda kosa hilo la mauaji.


"Ushahidi na vielelezo vilivyotolewa na upande wa mashtaka wameweza kuthibitisha bila kuacha shaka yoyote kuwa ametenda kosa, hivyo mahakama inawahukumu washtakiwa watano kunyongwa mpaka kufa isipokuwa mshtakiwa Kanungu ambaye ushahidi wa mashtaka haujamgusa". Amesema Jaji Kulita.


Katika kesi hiyo upande wa mashtaka uliwakilishwa na wakili wa Serikali Mwandamizi Credo Rugaju,  wakili wa serikali Lilian Lwetabura na Veronica Mtafya.


Katika kesi ya msingi washtakiwa kwa pamoja walidaiwa kuwa Novemba 3 mwaka 2013 huko Mbezi Msakuzi Kiswegere walimuua kwa kukusudia Dk.Sengondo Mvungi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...