WANANCHI wa kata yaMwarusembe wilayani Mkuranga mkoani Pwani wameahidiwa kujengewa kituo cha afya ndani ya miaka mitano ijayo. 

Ahadi hiyo imetolewa na mgombea ubunge Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega wakati alipokuwa akiomba kura mbele ya wananchi hao na kusema zahanati inayojengwa kwenye Kata hiyo imekamilika na itafunguliwa mwezi December mwaka huu baada ya uchaguzi. 

Ulega amesema miaka mitano ijayo wamejipanga kwenda kutekeleza shughuli za maendeleo na moja ya mikakati waliyonayo ni kuifanya zahanati ya mwarusembe kuwa kituo cha afya na gari ya kubebea wagonjwa italetwa.

Ulega ambaye ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ameongeza kuwa kikubwa cha kufanya kwa sasa ni kujenga nyumba ya mganga na  wodi ya kinamama ili kuwaondolea changamoto ya umbali kinamama wanapotaka kujifungua .

Aidha mgombea huyo amewatoa hofu wananchi hao kuhusiana na barabara yao ya  Bigwa -kiziko kuwa inaenda kukarabatiwa km 6 kwa kuweka kifusi na tuta kwenye sehemu korofi kwasababu imeingia kwenye bajeti ya serikali. 

"Katika miaka mitano hii tunaenda kukamilisha zahanati ya bigwa, muda mfupi ujayo umeme utafika kitonga nimeshazungumza na naibu waziri wa nishati Subira Mgalu na ndugu wa kinene tunajenga shule pale Ili watoto wetu wapate kusoma pale!". Amesema Ulega 

Akizungumzia aliyoyafanya miaka mitano iliyopita mgombea huyo amesema ukiacha ujenzi wa zahanati na madarasa ametoa mashine mbili za kufyatua tofali vibao mia na lory nne za mchanga lengo kuwainua vijana  kiuchumi 

Sanjari na hayo Ulega amesema katika miaka mitano hii aenaenda kukamilisha zahanati ya bigwa na muda mfupi ujayo umeme utafika kitonga na vijiji vingine vilivyobakia. 

Akizungimzia michezo wakati wa kampeni Ulega amesema, Ulega Cup itaendelea na vijana wote kila kijiji watapata jenzi na mpira,na vikundi vya kimama vitapewa kipaumbele katika suala zima la mikopo 

Aikiendelea na kampeni katika kata ya Kiparang'anda ameahidi kutoa 
 mil 1.5 kwajili ya ujenzi wa sehemu ya biashara ya wazee wa Matunda .

Hata hivyo bararabara ya Kibanda Baridi Msolokelo ipo kwenye orodha rasmi ya serikali pale chini na tutaweka karavati mbez - msokelo na kusema kuwa ataunga mkono zahanati zote zilozoazishwa na madarasa yatajengwa.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi leo Kata ya  Mwarusembe.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)





Mwanachama mpya wakipokea Kadi za CCM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...