Na Chalila Kibuda,Michuzi TV 


Wanawake wametakiwa kujiamini katika uongozi na kuacha kupewa nafasi za uongozi kwani kunafanya kukosa kujiamini.

Hayo aliyasema mgeni rasmi Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Huduma kwa Wateja Wakubwa wa Benki KCB Christina Manyenye wakati wa kufunga mafunzo ya Fifa ya Uongozi na Utawala katika Mpira wa Miguu yaliyofanyika ukumbi wa Shirikisho la soka Tanzania(TFF) Jijini Dar es Salaam.

Amesema wanawake kutoona mafunzo hayo kama ni jambo dogo bali wachukue kwa ukubwa na kusonga mbele hatua inayofuata katika kutimikia masuala ya uongozi.

Manyenye amesema uongozi wa mwanamke unatakiwa kuanzia ngazi ya familia na kwamba wanachotakiwa kufanya ni kujitambua, kujiamini na kutafuta fursa watakazoziona mbele bila kutegemea nafasi Bali inatakiwa kuonyesha uwezo.

“Kinachotuangusha wanawake wengi hatujiamini katika uongozi, mnatakiwa mbadilike kama ni changamoto huwa zipo na ndizo ambazo zinatusaidia kutuweka imara,”amesema Mnyenye 

Upande wa Mkufunzi wa kimataifa wa Fifa Henry Tandau amewahimiza wanawake waliohitimu mafunzo ya uongozi na Utawala wa mpira wa miguu kuchangamkia fursa zitakazojitokeza katika soka.

Tandau amesema mpango wa mafunzo ni endelevu wa kuwawezesha kushiriki katika uongozi nchi nzima.

Amesema anatamani kuona kati ya wahitimu hao, baadhi yao waje kuwa ni viongozi wakubwa akitolea mfano Rais na nafasi nyingine za juu huku akijivunia kuna baadhi ya viongozi walioko TFF aliwahi kuwafundisha na baada ya miaka kadhaa leo ni watu wakubwa katika uongozi.

“Ni matumaini yangu baadaye nitaona kati ya ninyi wapo watakaokuwa viongozi wakubwa. Lengo ni kuona na ninyi mnagombea nafasi mbalimbali, mnaweza kuwa viongozi kwenye klabu, vyama vya michezo na mashirikisho,”amesema.

Tandau amesema mafunzo hayo yameanza Dar es Salaam ila yataendelea mikoa mingine ya Tanga, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Mwanza, Unguja, Geita, Mbeya, Songea na Zanzibar.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa wahitimu ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio cha EFM Tunu Shenkome aliwashukuru TFF kwa kuwapa nafasi ya mafunzo hayo na kuahidi kile walichokipata watakwenda kukitumia katika taasisi zao.

“Tutakwenda kutumia kwa vitendo kile tulichokipata, naimani TFF wataendelea kutoa kozi hii kwa wengine ili kuwapata wanawake wengi katika uongozi wa soka,”amesema.

 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Huduma ya Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB Christina Manyenye akizungumza  wakati wa kufunga mafunzo ya wanawake katika Uongozi wa Mpira wa Miguu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

 Mkufunzi wa Kimataifa Henry Tandau akitoa maelezo kuhusiana na mafunzo ya wanawake 38 ya Uongozi na Utawala katika mpira ya Miguu ,jijini Dar es Salaam. 

Mgeni Rasmi Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Huduma ya Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB Christina Manyenye akimkabidhi cheti mshiriki wa mafunzo ya Wanawake ya Uongozi na Utawala Mtangazaji wa EFM Tunu Shenkome katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Huduma kwa Wateja Wakubwa wa Benji ya KCB, Christina Manyenye (mwenye gauni nyekundu )akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mafunzo ya Wanawake katika uongozi na Utawala wa mpira wa miguu ,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...