Na Mwandishi Wetu
JESHI la Zimamoto na Uokoaji nchini limewataka wamiliki wa shule nchini kuhakikisha wanafunga vifaa maalumu vya awali vya kuzimia moto ili kuweza kudhibiti majanga pindi yanapotokea na kupunguza athari za majanga hayo

Hayo yalisemwa na Kaimu Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, DCF Charo Mangare baada ya kutembelea Shule ya Msingi ya Byamungu Islamic iliyopo Kata ya Itera, wilayani Kyerwa mkoa wa Kagera ambapo kulitokea ajali ya moto na kusababisha vifo vya wanafunzi 10 na majeruhi sita.

“Pamoja na kuwaagiza wamiliki wa shule kufunga vifaa maalumu vya kudhibiti moto pia nawaagiza makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini kukagua shule zote na zoezi hilo liwe endelevu ili kuweza kudhibiti madhara ya ajali hizo pindi zinapotokea” alisema DCF Mangare

Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo DCF Mangare alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama inaendelea na uchunguzi na pindi utakapokamilika taarifa itatolewa kwa wananchi ili kuwepo sasa mbinu za kudhibiti ajali kama hizo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Muuguzi Mkuu Msaidizi, Justine Katalaiya alisema majeruhi wanne kati ya sita waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Karagwe wamehamishiwa Hospitali ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.

Kaimu Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, DCF Charo Mangare akifanya ukaguzi baada ya kuwasili eneo la tukio la ajali ya moto iliyosababisha vifo vya wanafunzi 10 katika Shule ya Msingi ya Byamungu iliyoko Kata ya Itera,Wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.
Kaimu Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, DCF Charo Mangare akimsikiliza Muuguzi Mkuu Msaidizi wa Hospitali ya Nyakahanga, Justine Katalaiya (kulia), juu ya hali ya mmoja wa majeruhi wa ajali ya moto iliyosababisha vifo vya wanafunzi 10 baada ya ajali ya moto katika Shule ya Msingi ya Byamungu iliyoko Kata ya Itera,Wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.
Kaimu Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, DCF Charo Mangare akimpa pole mmoja wa wazazi wa watoto waliokuwepo eneo la tukio la ajali ya moto iliyosababisha vifo vya wanafunzi 10 katika Shule ya Msingi ya Byamungu iliyoko Kata ya Itera,Wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.
Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...