Charles James, Michuzi TV
VIONGOZI mbalimbali akiwemo
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally, Katibu wa Itikadi na Uenezi,
Humphrey Polepole na Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma,
Mariam Ditopile wamejitokeza katika kituo cha kupiga kura cha Kilimani
jijini Dodoma kupiga kura ya kuchagua Rais, Mbunge na Diwani huku
wakieleza kuridhishwa na muamko wa wananchi pamoja na hali ya amani na
utulivu iliyopo.
Akizungumza baada ya kupiga kura Dk Bashiru
amewataka watanzania kuzidi kujitokeza kwa wingi kwenye vituo
walivyojiandikisha ili waweze kutimiza haki yao ya Msingi ya kuchagua
viongozi wanaowataka.
Kwa upande wake Polepole ameipongeza Tume
ya Taifa ya Uchaguzi NEC kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwapokea
wananchi na kuelekeza ili waweze kupiga kura bila usumbufu wowote.
"
Nimeridhika na hali ya utulivu, wananchi wamehamasika sana na uchaguzi
huu, niwaombe wanaokuja vituoni kupiga kura wakishamaliza warudi
majumbani mwao wasubiri matokeo," Amesema Ditopile.
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally akiwa kwenye foleni ya kupiga kura katika kituo cha Kilimani jijini Dodoma. Wa mwisho ni Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile.
Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura katika kituo cha kupiga kura cha Kilimani jijini Dodoma leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...