Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Songwe

*Asema hata Ilani ya Uchaguzi Mkuu imeelezea kwa kina kuhusu wazee

*Azungumzia pia umuhimu wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Songwe

MGOMBEA urais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amesema wazee wote nchini wataendelea kulindwa na Serikali huku akieleza kuwa hata Ilani ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 imefafanua vizuri kuhusu mikakati ya kuhakikisha wazee wote wanaendelea kuenziwa ikiwa pamoja na kuendelea kupata matibabu ya afya bure.

Akizungumza leo kwenye mkutano wake wa kampeni wa kuomba ridhaa kwa wananchi ili aendelee kuwa Rais kwa miaka mingine mitano akiwa na mkoani Songwe Dk.Magufuli amesema leo Oktoba 1 mwaka 2020 ni siku ya wazee duniani, hivyo haiwezi kupita bila kueleza chochote kwani watu wote ni matokeo ya wazee na kila aliyepo anajua uwepo wake ni matokeo ya wazee.

"Ndio maana Ilani ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 katika ukurasa wa 142 hadi ukarasa wa 143 umefafanua kuhusu wazee na watalindwa kwa nguvu zote.Katika kipindi cha miaka mitano Serikali imeendelea kuwatambua, kuwathamini na kuwajali wazee wote, wakati tunaingia madarakani mwaka 2015 wazee waliokuwa na vitambulisha kwa ajili ya matibabu walikuwa  300,000 lakini hivi sasa wenye vitambulisho ni 1,423,000.

"Pia tumedhibiti mauaji ya wazee na hasa Kanda ya Ziwa baada ya kuvielekeza vyombo vya ulinzi na usalama kusimamisha ulinzi na usalama wazee.Tumeboresha makazi ya wazee katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya Nunge , Magugu, Fungafunga  kule Mara, na maeneo mengine. Hii ni kuthibitisha tutaendelea kuwa na wazee kwani hawajapitwa na wakati, maana wao wamefaidi nyakati zote,"amesema Dk.Magufuli.

Amesisitiza Ilani ya Uchaguzi inatoa muongozo wa kuendelea kuwalinda wazee na kuwathimini huku akifafanua anaelewa bado kuna baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili wazee lakini wataendelea kuzipatia ufumbuzi."Hata mimi mama yangu ni mzee ana umri wa miaka zaidi ya 80 , yuko kitandani hawezi kula wala kuzungumza, hivyo niwahakikishie tutaendelea kuwalinda wazee wetu wote,"amesema Dk.Magufuli.

Wakati huo akiwa anazungumza na wananchi wa Tunduma mkoani Songwe, Dk.Magufuli amewakumbusha Oktoba mwaka 2019 alifika Tunduma kwa ajili ya kuzindua kituo cha huduma za pamoja mpakani akiwa na Rais wa Zambia , hivyo leo hakutegemea kutakuwa na watu wengi wakimsubiri kwani wamejaa kulikoa alivyokwenda mwaka jana.

"Nimekuja kuomba kura leo, kama mnavyofahamu miaka mitano iliyopita tumeshirikiana kwa karibu na kufanya mambo mengi, nilikuwa Vwawa kabla ya kufika Tunduma na nimesema Mkoa wa Songwe unategemewa kwa uzalishaji chakula nchini na unashika nafasi ya tatu kwa uzalishaji."Nimeeleza tulivyojipanga kuendeleza suala la kilimo na nimeeleza Mkoa huu ni kitinda mimba, na nilimteua Mkuu wa Mkoa wa kwanza mwaka 2016, mkoa huu nauona kama mtoto wa mwisho anayependwa na wazazi, nawathibitisha Songwe nawapenda sana.

"Ilikuwa ngumu kwenda katika mikoa yote kufanya kampeni lakini nimeona Songwe lazima nikanyagae.Katika miaka mitano katika biashara nilikuja kuzindua kituo cha pamoja na huduma za mpakani ambacho kilianzishwa kwa ajili ya kuimarisha huduma za kibiashara mpakani.Ninyi watu wa Tunduma ni mashahidi kabla ya ujenzi na uzinduzi wa kituo hiki, watu walikuwa wanatumia hadi wiki mmoja kwa ajili ya kuvuka mpakani lakini sasa mambo safi, nataka kuwaahidi bado kuna changamoto tutazitatua,"amesema Dk.Magufuli.

Ameongeza katika biashara upande wa Tanzania wamejitahidi kurekebisha hata kero zilizokuwa zinawasumbua wafanyabishara wamefanikiwa kuzishughulikia kwa kiwango kikubwa na katika kipindi cha miaka mitano wamefuta tozo 104 katika sekta ya mifugo,kilimo na uvuvi na katika biashara wamefuta tozo 54, hivyo  kwa ujumla wamefuta tozo za kero  168 na kipindi kinachokuja wataendelea kuziondoa tozo ambazo ni kero.Amesema wanataka kujenga Tanzania mpya.Pia wanataka kuwawezesha Watanzania kufanyabiashara zao bila kusumbuliwa na hiyyo ndio dhana ya kuondoa umasikini

"Mwaka 2015 baada ya kuingia mdarakani alikuta wafanyabishara wadogo wakisumbuliwa, walikuwa wanafukuzwa kila wanapotaka kufanya biashara, walikuwa wanataseka.Tukasimama na kusema wafanyabiashara wadogo ili wawe wakubwa lazima walindwe na Serikali, tukaamua kuanzisha vitambulisho vya wajasiriamali ambavyo kuvitengeneza kuna gharama yake na tukaona ni vema wakatoa Sh.20,000 kuchangia gharama ya kukitengeza.

"Vitambulisho hivyo vimeleta unafuu mkubwa kwani hapo awali watu walikuwa wanatozwa hadi Sh.2000 kwa siku na kwa mwezi inakuwa Sh.60,000 na kwa mwaka inakuwa ni fedha nyingi.Hivyo tukaona tutoe vitambulisho ili wajasiriamali wafanye biashara bila matatizo na mahali kokote wanakotaka. Unaweza kufanya hapa biashara au Sumbawanga ama Dar es Salaam bila kusumbuliwa.

"Vitambulisho hivi vimesaidia hata wafanyabiashara wadogo kushirki katika uchumi wa Tanzania na ifahamike wamefanya hivyo kwa nia njema, ndio maana wenye bodaboda wanaweza kwenda kokote. Wasitokee watu wakawarubuni kuwa vitambulisho hivi havina maana,"amesema Dk.Magufuli wakati akielezea mikakati ya Serikali katika kuwalinda wafanyabiashara wadogo nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...