Na.Vero Ignatus ,Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe amewahakikishia wakazi wa Longido kwamba ulinzi na Usalama umeimarishwa hivyo wasiogope kwenda kupiga kura
Akizungumza katika kata ya

Namanga wakati wa kuhitimisha Kampeni aliwataka wananchi wa hao kwenda kupiga kura kwa wakati na asiwepo hata mmojawapo atakayekwenda kupiga kura akiwa amevaa sare yeyote ya chama cha siasa

Aliwataka wananchi hao warakapokwenda kupiga kura wahakikishe wanarudi nyumbani na kuendelea na shughuli nyingine n asiyo kukaa kituoni hapo

Akizungumza wakati wa kufunga Kampeni aliyewahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha Daniel Ole Njoolai alisema kuwa Chanda chema huvikwa Pete hivyo wakumbuke mema aliyowatendea Dkt.Magufuli hivyo wampatie kura ya ndiyo ashinde kwa kishindo.

Alisema Jimbo hilo lilikuwa na changamoto nyingi Ikiwemo tatizo la maji ambapo serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt.Magufuli imewezesha kutekeleza kwa mradi mkubwa wa maji, ujenzi wa hospitali ya wilaya pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo

Kwa upande wake Mgombea ubunge wa Jimbo hilo,Dkt.Steven Kiruswa,aliahidi kutokuwangusha wananchi wa Jimbo hilo Katika kipindi cha miaka mitano ijayo kwani katika kipindi cha miaka miwili iliyopita aliwezesha kufanyika miradi mbalimbali Ikiwemo ya maji,Elimu na Afya.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...