Na Lusajo Frank DSJ 
KLABU ya Manchester United yaiadhibu Paris saint German kwa kipigo cha goli mbili kwa moja, mhezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya uliopigwa katika dimba la Parc de Princes nchini Ufaransa.

United walipata goli la kwanza dakika 24 kupitia kwa Bruno Fernandez baada ya Antony Martial kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na walinzi wa PSG, mpaka kipindi cha kwanza kumalizika.


PSG walirejea kwa kasi kipindi cha pili na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha baada ya Antony Martial kujifunga dk 55, Rashford alikandamiza msumari wa moto dakika 87 na kuipa United bao la ushindi.

Hii ni mara pili PSG wanapokea kipigo kutoka kwa Manchester United, ikumbukwe mara mwisho timu hizo kukutana PSG walipokea kipigo cha goli tatu kwa moja, Parc de Princes.

United ipo nafasi ya pili akiwa na alama sawa na Rb Leipzig wakitofautiana magoli katika kundi H.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...