NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza

WATU sita wamekamatwa wilayani Ukerewe wakidaiwa kuchoma nyaraka mbalimbali za ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kagunguli.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuulizwa na gazeti hili kuhusu tukio hilo.

Alisema watu sita bila kuwataja majina, wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Ukerewe kwa tuhuma za kuvunja mlango wa jengo la ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kagunguli na kuchoma nyaraka mbalimbali za ofisi hiyo.

“Watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuchoma karatasi (nyaraka) mbalimbali kwenye ofisi hiyo ya Mtendaji wa Kata kwa hisia kuwa kulikuwa na karatasi za ziada za kupigia kura,kabla ya kufanya tukio hilo walivunja mlango wa jengo hilo lenye ofisi sita,”alisema Muliro. Alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilika litawafikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria ili kujibu tuhuma zinazowakabili..

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana nahali ya usalama kabla na baada matokeo ya uchaguzi mkuu jana. Na Baltazar Mashaka



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...