Na Shukrani Kawogo, Njombe.

Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga ameendelea na kampeni za kumuombea kura rais John Pombe Magufuli pamoja na madiwani ambao  hawajapita bila kupingwa ambapo kwa sasa ameanza kutembelea kata zilizopo katika tarafa ya Mwambao.

Katika tarafa hiyo mbunge huyo ameanza na kijiji cha Nkwimbili kilichopo katika kata ya Lupingu ambacho kimezungukwa na safu ya milima Livingston huku kikiwa na wakazi zaidi ya elfu tatu.

Akiwa njiani kuelekea katika kijiji hicho Kamonga amesema kuwa amejionea mwenyewe  tabu wanayoipata wakazi wa kijiji hicho kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara hivyo ana kila sababu ya kutafutia ufumbuzi suala hilo.

Alisema wakazi wa eneo hilo wanalazimika kutembea kwa umbali wa zaidi ya kilometa 5  kufuata huduma mbalimbali pamoja na kufika katika vijiji vingine.

" Nikiwa kama kiongozi napaswa kujua changamoto wanazokabiliana nazo wananchi wangu, kwakweli kutembea kwa kupanda mlima zaidi ya masaa mawili si kitu kidogo tena ukizingatia wanapandisha huku wakiwa na mizigo kichwani", Alisema Kamonga.

Alisema tatizo hilo amelichukua kama changamoto inayohitaji kutatuliwa hivyo atahakikisha barabara inatengenezwa ili wananchi hao waweze kwenda maeneo mengine kwa kutumia pikipiki.

Aidha alipokuwa anakaribia kufika katika kijiji hicho alikuta bendera ya Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) ikipepea katika nyumba ya mmoja wa wakazi hao ambapo mkazi huyo baada ya kumuona mbunge huyo kafika katika kijiji chao alishusha bendera na kutangaza kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mkazi huyo aliyejulikana kwa jina la Apronistoli Mwakalago lisema kuwa ameamua kufanya maamuzi hayo kutokana na furaha aliyonayo juu ya mbunge huyo kwani hakutegemea kama atafika katika kijiji chao.

Aliongeza kuwa viongozi wengi wamekuwa hawafiki katika kijiji chao kutokana na kufika kwake kunategemea kutembea na kupanda milima hivyo wanaamua kuwaacha.

" Nimefurahi kuona mbunge wetu Kamonga amefika huku kwetu, hii ni ishara njema kwetu na ninaamini kupitia uongozi wake na sisi tutapata maendeleo hasa katika uboreshaji wa barabara", Alisema Mwakalago

Mbunge huyo ambaye alianza kampeni hizo Octoba 3 mwaka huu na  mpaka sasa tayari ametembelea kata 22 kati ya 26 na anatajia kuhitimisha kampeni hizo Octoba 27 mwaka huu.

Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kulia akikunja bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)baada ya kukabidhiwa na mwanachama wa chama hicho Apronistoli Mwakalago Katika kijiji cha Nkwimbili kata ya Lupingu wilayani Ludewa.
Mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Apronistoli Mwakalago akishusha bendera ya chama hicho baada ya kufurahishwa na kufika kwa mbunge huyo katika kijiji chake na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa kwenye picha ya pamoja na wananchi wa Kijiji cha Nkwimbili huku wakiwa wamenyoosha mikono juu wakionyesha ishara ya miaka mingine mitano ya rais John Pombe Magufuli.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (wakwanza kushoto) akizungumza na mkazi wa kata ya Nkwimbili aliyefahamika kwa jina la Anna Nkwera baada ya kukutana nae akipanda mlima huku akiwa na ndoo ya maji kichwani, kulia ni mgombea udiwani wa kata ya Lupingu Scander Mwinuka
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi na wanachama  wa CCM wakipanda mlima kuelekea Kijiji cha Nkwimbili kata ya Lupingu wilayani Ludewa kwenda kumuombea kura rais John Pombe Magufuli.

Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa na vijana wake wakipandisha mlima kutoka Kijiji cha Lupingu wakielekea kijiji cha Nkwimbili kata Lupingu katika mkutano wa kumuombea kura rais John Pombe Magufuli.
Nyumba za wananchi wa Nkwimbili zikionekana kwa mbali katika safu ya milima Livingston ambako mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga alifika kwenda kumuombea kura rais John Pombe Magufuli na mgombea udiwani wa kata ya Lupingu.
Mgombea udiwani wa kata ya Lupingu Scander Mwinuka akiwa sambamba na mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (mwenyewe nguo ya njano) pamoja na Diwani mteule wa kata ya Ludende Vasco Mgimba (Mwenye nguo ya kijani) na Diwani mteule wa kata ya Ibumi Edward Haule wakishuka mlima wa Nkwimbili baada ya kumaliza mkutano wa kumuombea kura rais John Pombe Magufuli na diwani wa kata ya Lupingu.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga ( Mwenye nguo nyeupe kushoto) akiwa na timu yake wakipumzika baada ya kutembea kwa muda mrefu wakitokea kijiji cha Lupingu kuelekea kijiji cha Nkwimbili kata ya Lupingu wilayani Ludewa.
Mbunge mteule Joseph Kamonga akitelemka katika mlima wa Kijiji cha Nkwimbili kata ya Lupingu kuelekea kijiji cha Lupingu baada ya kumaliza mkutano katika kijiji hicho.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...