Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwaonyesha  baadhi ya wananchi wa kata ya Pangani ilani ya Chama cha mapinduzi (CCM) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali kwa kipindi kingine cha miaka mitano wakati wa mkutano wake wa kampeni kwa ajili ya kuomba kura ili aweze kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu.

Mwonekano wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya CCM Silvestry Koka akizungumza na wananchi  kutoka mitaa mbali mbali ya kata ya pangani  ikiwa ni mkutano wake wa kampeni kwa ajili ya kuweza kuomba kura kwa wananchi hao.

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi katika halmashauri ya Mji Kibaha Maulid Bundala akiwa anafafanua jambo katika mkutano huo wa kampeni kwa ajili ya kuwanadi wagombea mbali mbali wa nafasi z aUrasi Ubunge pamoja na Udiwani.

Mgombea wa nafasi ya Udiwani wa katika kata ya Pangani Augustino Mdachi wa kulia akiwa amesimama katika jukwaa moja na Mgomea Ubunge wa Jimbo la Kibah mjini Silvestry Koka wakati wa kuomba kura kwa wananchi wa kata ya Pangani.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

****************************************

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Silvestry Koka ameahidi kulivalia njuga suala la changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi wanaoishi katika Kata ya Pangani ili kuondokana na adha ya kutembea umbari mrefu usiku na mchana kwa ajili ya kwenda kutafuta maji katika maeneo mengine .

Koka aliyasema  hayo wakati akizungumza na baadhi ya wananachi kutoka mitaa mbali mbali ya Kata ya Tanginini wakati wa mkutano wake maalumu wa kampeni wenye lengo la kunadi sera zake pamoja na kuomba kura kwa wananchi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba 28 mwaka huu.

Mgombea huyo aliongeza kuwa lengo lake kubwa endapo wananchi watamchagua tena kuongoza katika kipindi cha miaka mitano mingine kipaumbele chake kikubwa ni kuhakikisha anawaondolea tatizo la ukosefu wa maji na kwamba kuna fedha ambazo zimeshatolewa  na serikali kwa ajili ya miradi mbali mbali katika maeneo mbali mbali.

“Natambua kuna baadhi ya maeneo katika Kata ya Pangani kuna changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama lakini katika kipindi kilichopita nilishapambana kuhakikisha kwamba mradi wa maji unakuwepo kwa ajili ya kuweza kuwanufaisha wananchi wa mitaa mbali mbali na kwamba leo nimeweza kupata fursa ya kutembelea matanki makubwa ambayo yataweza kuwa na ujazo wa lita nyingi zzinazoweza kuondoa kabisa tatizo hili la maji.

Aidha Koka alisema kwamba kuna baadhi ya maeneo mengine katika kata ya Pangani yameshafaidia na huduma ya maji safi na salama hivyo sehemu ambazo bado hazijasambaziwa maji lazima zitapata maji kutokana na juhudi ambazo ameshazifanya katika kipindi kilichopita kwa kushirikiana na serikali ili kuona wananachi wanaondokana na hali ya usumbufu kila kukicha.

Akizungumzia suala la miundombinu ya barabara  Koka alifafanua kwamba nia na madhumuni yake ni kuhakikisha anaboresha baarabara mabli mbali za mitaa ili ziweze kufanyiwa ukarabati na hatimaye kuweza kupitika kwa urahisi katika kipindi chote hasa katika kipindi cha mvua zinaponyesha kwani kumekuwepo na  chanagmoto katika baadhi ya miundombinu kuharibika.

 Kwa upande wake Mgombea Udiwani wa kata ya Pangani Augustino Mdachi alisema kwamba katika kata yake kwa kipind miaka ya nyumba kulikuwepo na chnagamoto mbali mbali lakini kutoka na juhudi amabzo alizifanya kwa kushirikiana na wananchi wake waliweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta mbali mbali za afya elimu pamoja hudumu nyingine za kijamii.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Halmashauri ya Wiaya ya Kibaha mji Maulid Bundala aliwawataka wananchi kuhakikisha wanafanya maaamuzi ambayo ni sahihi kwa kuwachaguz viongozi wa ccm ambao wanaweza kuwaletea mabadiliko ya kimaendeleo kutokana na kutimiza yale yote ambayo yameandika katika utekelezaji wa ilani ya chama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...