Diwani Mstaafu wa Kata ya Mzimuni Mohamed Chambuso akimnadi Mgombea Udiwani wa kata hiyo Manfred Lyoto katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mtambani Magomeni.
Mgombea Udiwani Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mtambani ikiwa kuomba kura ya kuchaguliwa Diwani katika kata hiyo.
Meneja wa Kampeni wa Mgombea Udiwani Kata ya Mzimuni Abdallah Kitumbi akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto katika mkutano wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mtambani Magomeni.
Vijana wa hamasa wakiweka vibwagizo Katika mkutano wa kampeni.
Katibu wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Hemed Salum 'DEDY' akizungumza kuhusiana na vijana katika kutumia haki ya kupiga kura katika maendeleo ya nchi kwa kutanguliza maslahi ya Chama hicho katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mtambani, Magomeni

Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni ya Mgombea Udiwani kata ya Mzimuni.


Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto amesema kuwa akichaguliwa kuwa Diwani wa Kata hiyo  katika uchaguzi mkuu utaofanyika kesho Oktoba 28, 2020 katika ahadi zake ni pamoja na kutatua tatizo la mafuriko baadhi ya maeneo ya kata ya Mzimuni.

Akizungumza katika mkutano wa  kampeni uliofanyika katika viwanja vya mtambani Lyoto amesema kuwa Teknolojia zimekuwa na kupitia watalaam wataweza kuweka miundombinu ya maji vizuri na kufanya wananchi wasiathirike na hayo.

Lyoto amesema  akichaguliwa atahakikisha kata ya Mzimuni inakuwa kitovu cha kujifunza katika nyanja ya maendeleo kwa kutumia uwezo na mbalimbali  kushirikisha wadau katika ufadhili wa miradi.

Hata hivyo amesema wananchi wasipoteza kura yao katika uchaguzi ili anachofikiria kiweze kutekelezeka kwa vitendo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...