Mgombea Udiwani wa Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto akizungumza katika mkutano wa Kampeni katika wiwanja vya Mwinyi Mkuu Magomeni Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Kampeni wa Mgombea Udiwani kata ya Mzimuni Abdallah Kitumbi akimnadi Mgombea Udiwani wa kata hiyo (hayuko pichani) katika viwanja vya Mwinyi Mkuu Magomeni wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Mzimuni Hemed Salum 'DEDY' akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata hiyo katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mwinyi Mkuu Magomeni Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Vijana wa hamasa wakisherehesha wakati wa kampeni hizo.


 Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni.

 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam .

MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto amesema kuwa akichaguliwa kuwa diwani atafanya mikakati ya kuhakikisha wanafunzi  wa kata hiyo wanapata chakula wakiwa shuleni. 

Lyoto amesema hayo wakati wa kampeni zilizofanyika katika viwanja vya Mwinyi Mkuu Magomeni wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Amesema, kitu hicho hakiwezi kufanywa na wengine  na ameahidi uwepo wa chakula katika shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika kata hiyo pindi tuu atakapochaguliwa.

Pia, Lyoto amesema Kata ya Mzimuni haina taa katika barabara za mitaa, hivyo akichaguliwa ataweka taa na sio kutegemea taa zinazowaka katika nyumba za wananchi kumulika barabara.

Hata hivyo amesema kuwa Chama kimekuwa na Ilani ya kuboresha maisha ya wananchi katika kupata huduma hivyo wasifanye makosa katika uchaguzi wa Oktoba 28.

Lyoto amewataka wananchi kujitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura kwa kuzingatia mfumo wa Utatu 'mafiga matatu yaani kwa kuchagua Rais wa CCM, Mbunge wa CCM pamoja na Diwani wa CCM.

"Wananchi nichagueni hivi vitu ambavyo nimevipanga kuvifanya niweze kufanya nikiwa Diwani na tutakwenda sawa."amesema Lyoto.

Mwenyekiti wa Kata ya Mzimuni Hassan Yahaya Hussein  amesema kuwa kuwa mgombea Udiwani ni mtu mahiri  na msomi hivyo ataweza kwenda na kasi.

Meneja wa Kampeni Abdallah Kitumbi amesema kuwa wananchi wanataka maendeleo hivyo Mgombea yupo tayari kusimamia changamoto na kuzitatua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...