Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi alipowasili katika mkutano wa kampeni za uchaguzi Mkuu uliofanyika leo katika Uwanja wa Dole Wilaya ya Magharibi”A”{Picha na Ikulu} 22/10/2020.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akihutubia na kumnadi Mgombea wa Urais wa Zanzibar,Wabunge.Wawakilishi na Madiwani   katika mkutano wa kampeni za uchaguzi Mkuu wa Wilaya ya Dimani na Mfenesini Kichama uliofanyika leo katika Uwanja wa Dole Wilaya ya Magharibi”A”. {Picha na Ikulu} 22/10/2020.  Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya  ya Dimani na Mfenesini  kichama wakiwa katika katika mkutano wa kampeni za uchaguzi Mkuu uliofanyika leo katika Uwanja wa Dole Wilaya ya Magharibi”A” ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).{Picha na Ikulu} 22/10/2020. 

Wagombea Ubunge na Uwakilishi wa Wilaya  ya Dimani na Mfenesini  kichama wakienda kutunza wakati wa utenzi uliosomwa na KIJANA wa CCM Hajra Fadhil (hayupo pichani) katika mkutano wa kampeni za uchaguzi Mkuu uliofanyika leo katika Uwanja wa Dole Wilaya ya Magharibi”A” ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.{Picha na Ikulu} 22/10/2020.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiwanadi Wagombea wa Ubunge.Uwakilishi na Madiwani   katika mkutano wa kampeni za uchaguzi Mkuu wa Wilaya ya Dimani na Mfenesini Kichama uliofanyika leo katika Uwanja wa Dole Wilaya ya Magharibi”A”. {Picha na Ikulu} 22/10/2020.  Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi alipokuwa akiwapungia mkono wanaCCM mara alipowasili katika viwanja vya mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu Dole Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi  uliofanyika leo katika Uwanja wa Dole Wilaya ya Magharibi”A”,[Picha na Ikulu] 22/10/2020. 

****************************************

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema endapo atapata ridhaa ya wananchi na kuwa rais, ataimarisha maslahi ya watumishi wa umma kwa kuongeza mishahara na posho kwa wakati.
Aliwataka wafanyakazi hao wa umma kuwa tayari kufanya kazi kwa bidii kwani wataboteshewa maslahi yao lakini watafanya kazi kwa kasi zaidi.
Ahadi hiyo aliitoa katika mwendelezo wa kampeni za CCM za kuwanadi wagombea wa CCM na kufafanua Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 huko katika kiwanja cha Dole Unguja.
Alisema mbali na kuimarisha maslahi ya makundi yote ya kijamii ikiwemo maslahi ya watumishi wa umma, pia atapitia upya maslahi ya wastaafu ili wapate pencheni kubwa kuliko wanayopata hivi sasa.
Aliwambia wananchi kuwa atalinda umoja wa kitaifa na kudhibiti vitendo vya ubaguzi wa kidini,kisiasa,kikabila.
“Nitadhibiti vitendo vya ukabila hapa kwetu kuna Upemba na Uunguja yote hayo nitayaondosha ili wote tuendelee kuwa wamoja”,alisema Dk.Hussein.
Dk.Hussein,alisema anaipongeza serikali ya awamu ya saba kwa hatua kubwa iliyopigwa katika sekta ya elimu kwa kujenga skuli za kisasa zenye vifaa vya masomo ya sayansi katika Mkoa huo
Alisema licha ya mafanikio hayo bado kuna changamoto za uchache wa madarasa na madawati mambo yanayotafutiwa ufumbuzi.
Alisema pia kuna upungufu wa walimu wa sayansi na masomo mengine chanfamoto itakayotafutiwa ufumbuzi.
Alisema serikali hiyo imejenga vituo vya afya vya kisasa vinavyotoa huduma bora kwa wananchi.
Alisema katika mkoa huo kuna vyanzo vingi vya maji safi na salama licha ya kuwepo na changamoto ya ubovu na uchakavu wa baadhi ya miundombinu na zitatafutiwa ufumbuzi.
Alitumia mkutano huo kujiombea kura na kuwaombea kura wagombea wote wa CCM aliwemo Dkt.John Pombe Magufuli.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alisema Zanzibar  imekuwa huru toka mwaka 1964 baada ya kufanyika mapinduzi ya mwaka 1964 na kwamba wananchi wanatakiwa kulinda tunu hiyo kwa kuichagua CCM.
Alisema mapinduzi hayo ni kielelezo tosha cha kulinda muungano na amani ya nchi.
Alisema mapinduzi hayo ndio msingi wa maendeleo ya nchi.
Alieleza kwamba baada ya mapinduzi serikali iliyoongozwa na rais wa kwanza marehemu Abeid Aman Karume,iliasisi mikakati ya maendeleo zikiwemo sera za elimu, bure,afya bure na kugawa ardhi bure kwa wananchi.
Katika maelezo yake Dk.Shein,alikemea vitendo vya kuwajeruhi wanachama wa CCM vinavyofanyika nchini katika maeneo mbalimbali na kuviita ni vitendo vya kihuni visivyofaa katika siasa za vyama vingi.
Alisema vyama vya siasa vishindane kwa sera na sio kuumizana kwani vitendo hivyo vinaweza kusababisha machafuko ya kisiasa.
Alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni ya kiungwana wala haina malengo ya kuwaumiza wananchi badala yake itaendelea kufuata Katiba ya nchi na sheria ili kuendeleza amani iliyopo.
Aliwataka wananchi kuwa na amani na wajitokeze kwa wingi kupiga kura ifikapo octoba 28,mwaka huu kwani ulinzi umeimarishwa kila sehemu.
Pamoja na hayo Dk.Shein,aliwaombea kura wagombea wa wa Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi za Urais ,Ubunge,Uwakilishi na madiwani.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,amesema CCM inalaani vikali vitendo vya uvunjifu amani vinavyofanywa na watu wanaosadikiwa kuwa wapinzani vya kuwajeruhi wanachama wa chama hicho.
Dk.Mabodi, alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua stahiki za kuthibiti vitendo hivyo visiendee na kwamba CCM haitolipiza kisasi bali itaendelea kudai amani mpaka wanashinda kwa kura nyingi na kuingia ikulu.
Alisema CCM imefanikiwa kuwafikia wananchi wa makundi mbalimbali katika kampeni zake kwa lengo la kueleza sera imara na kuwaomba kura ili waichague ifikapo octoba 28 ,mwaka huu.
Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi Taifa ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa Magharib kichama Dkt.Edmund Mndolwa amesema  sababu ya CCM kushinda ni kuwa na ilani inayotekelezeka ambayo ndio mkataba wa CCM na wananchi muongozo ambao umetekelezwa kwa ufanisi mkubwa.
Alisema wananchi wanatakiwa kuichagua CCM ili kuwapa fursa viongozi wa CCM wamalizie miradi na mambo ambayo walikuwa hawajamaliza katika ilani iliyopita na yamaliziwe katika ilani mpya.
Alisema wananchi wanatakiwa kulinda amani ya nchi ili nchi iendelee kupiga hatua kubwa za kimaendeleo ambapo Tanzania imekuwa ni kisiwa cha amani barani afrika.
Alisema Tanzania ni nchi ya 28 kwa kutumia vizuri fedha za umma kwa maendeleo ya taifa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Magharib kichama, Mohamed Rajab Soud alisema katika uongozi wa serikali ya awamu ya saba chini ya Dk.Ali Mohamed Shein amejenga vituo vya afya vilivyosaidia kupunguza usumbufu kwa wananchi kufuata huduma za afya nje ya mkoa huo.
Alisema mkoa huo kwa sasa unang’ara kwa miundombinu ya barabara za lami kila sehemu hali inayosaidia kuwarahisishia wananchi kusafiri kwa haraka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Alisema ungozi huo pia umejenga shule mbalimbali za ghorofa zenye miundombinu mbalimbali.
Mkutano huo umezishirikisha wilaya mbili ambazo ni Mfenesini na Dimani kichama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...