Mkurugenzi Msaidizi, Huduma na Ufuatiliaji wa Wizara ya Maji Mhandisi Lyidia Joseph akiongea na wajumbe wa bodi pamoja na wadau wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA), hawapo pichani, wakati akizindua bodi ya saba ya mamlaka hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA) Mhandisi Mbike Jones akisoma taarifa ya utekelezaji ya KUWASA kwa wadau na wajumbe wapya walioteuliwa kusimamia mamlaka hiyo mjini Kigoma.

Mratibu wa Kanda wa Mamlaka za Maji kutoka Wizara ya Maji Mhandisi Edwin Raphael akiongea kuhusu mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa utekelezaji wa majukumu kwa wajumbe wapya wa Bodi ya KUWASA walioteuliwa hivi karibuni, ambapo amesisitiza kuongeza mtandao wa maji kwa wananchi na kuzuia upotevu wa maji ni jambo la msingikatika kufikia malengo.

Sehemu ya wadau wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA) waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya saba ya mamlaka hiyo mjini Kigoma.

Mhandisi Lyidia Jospeh, pamoja na wadau na bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA) wakiangalia mtambo wa kusukuma maji wa KUWASA, eneo la Amani Mjini Kigoma.

Na Mwandishi wetu, Kigoma.

* Yaelezwa KUWASA inatekeleza Miradi ya Maji ya Bilioni 49.7

SERIKALI inatekeleza miradi mbalimbali ya maji yenye thamani ya shilingi bilioni 49.7 kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma na Ufuatiliaji wa Wizara ya Maji Mhandisi Lyidia Joseph. 

Amesema hayo kwa niaba ya Mhandisi Sanga wakati akizindua bodi mpya ya muhula wa saba ya KUWASA baada ya ile ya awali iliyoanza kazi mwezi Julai 2016 muda wake Juni 2019.

Akizindua bodi hiyo mpya Mhandisi Lyidia amesema zipo changamoto zinazohitaji utatuzi hivyo kuitaka bodi mpya kujipanga na kuendeleza jitihada zilizofikiwa na bodi iliyopita na kuhakikisha misingi ya uendeshaji wa mamlaka inaimarika.

Amesema Serikali imejipanga kumaliza changamoto ya huduma ya maji mkoani Kigoma ambapo ipo miradi inayotarajiwa kuanza itakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 9.8, ikiwamo ujenzi wa kitekeo kipya cha maji katika eneo la ufukwe la Amani, ukarabati wa miundombinu ya mradi wa maji Mwandiga na mradi wa uondoaji majitaka Manispaa ya Kigoma.

Bodi mpya ya KUWASA imetakiwa kutumia nyenzo iliyokabidhiwa kuwa kichocheo katika kurahisisha utekelezaji wa majukumu, ikiwemo Sheria ya Maji Na. 5 ya mwaka 2019, na Mpango wa Biashara wa Mamlaka kwa mwaka 2019/2020-2021.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...