Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Tike Mwambipile akizungumza na waandishi wa habari katika warsha iliyowakutanisha, ambapo ameeleza majukumu ya TAWLA na mafanikio yao katika miaka 30 wanayoadhimisha Novemba mwaka huu, Tike amesema kuwa TAWLA itaendelea kumlinda na kumtetea wanamke watoto, leo jijini Dar es Salaam.

Mwanahabari mkongwe Edda Sanga akitoa somo kwa waandishi wa habari katika warsha hiyo, pamoja na kujadili changamoto za kisheria zinazowakumba wanawake Edda amewataka wanahabari kuendelea kufuata miiko ya kazi hiyo ikiwa ni pamoja na kutumia vyema kalamu zao katika kuonesha umuhimu wa kuwa na usawa wa kijinsia katika nyanja zote, leo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wanahabari wakiwa katika matukio mbalimbali ya warsha hiyo iliyoandaliwa na TAWLA ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Chama hicho, leo jijini Dar es Salaam.

* Wanahabari watakiwa kuendelea kuzingatia maadili ya kazi yao

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IKIWA ni maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwake, Chama cha wanasheria  wanawake nchini (TAWLA,) kimeeleza azma yake ya kuendeleza jitihada za kutetea haki za mwanamke hasa kwa kutoa msaada kwa kisheria kwa makundi ya wanawake na watoto.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Tike Mwambipile katika warsha iliyowakutanisha na wanahabari jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wanahabari kuzingatia maadili ya uandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kuripoti matukio kandamizi kwa jamii hasa unyanyasaji wa kijinsia na vitendo vingine vya kikatili.

Amesema kuwa TAWLA wamekuwa wakifanya tafiti na kusimamia miradi mbalimbali na matamanio yao ni kuona idadi ya wanawake ikiongezeka katika ngazi mbalimbali za uongozi ikiwemo katika nyanja za siasa, taasisi za Umma na binafsi.

Amesema kuwa kwa miaka 30 wanajivunia mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wanawake wanasheria kukua kitaaluma, kuwasaidia wanawake katika masuala ya kisheria na hadi sasa tayari wamefungua ofisi katika kanda tano (Dar es Salaam, Tanga, Dodoma,Mwanza, Arusha na Mbeya.) Ofisi ambazo zinafanya kazi ya kuhakikisha haki za wanawake na watoto hazivunjwi kwa namna yoyote.

Aidha amesema kuwa TAWLA wanashirikiana kwa karibu na Serikali na wadau katika kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kupiga vita vitendo vya ukatili na kutoa misaada ya kisheria kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, na kueleza kuwa wataendelea kuwafikia walengwa wengi zaidi.

Kwa upande wake mwanahabari mkongwe nchini Edda Sanga ameipongeza TAWLA kwa kuendelea kutetea kundi la wanawake linalokumbana na vitendo vya unyanyasaji vinavyowaathiri na kutengeneza taifa la watu wasiojiamini.

Amesema kuwa ni wajibu wa kila mmoja katika jamii kuhakikisha jamii hiyo hasa wanawake na watoto inakua salama wakati wowote dhidi ya vitendo vyovyote vya ukatili.haba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...