Na Lusajo Frank DSJ 

RAIS wa zamani Burundi, Pierre Buyoya amehukumiwa kifungo cha maisha jela bila yeye mwenye kuwepo katika hukumu ya mauaji  ya mtangulizi wake, Rais wa nchi hiyo Melchoir Ndadaye mwaka 1993.

Kwa mujibu wa uamuzi wa mahakama ulioonyeshwa kwa shirika la habari la AFP, Buyoya alihukumiwa kwa kosa la kumshambulia Rais wa Burundi ambaye alichaguliwa kidemokrasia katika nchi ya Burundi.

 Ndadaye, wakati huo aliondolewa madarakani baada ya   kuitumbukiza serikali yake vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tofauti  na Buyoya, maafisa wengine 18 waandamizi wa kijeshi na raia wa Burundi  walikuwa karibu naye wamepewa hukumu ya kifungo Maisha Jera.

Wengine watatu wamehukumiwa miaka 20 jela kwa Uzembe katika uhalifu. 

Ingawa  Waziri mkuu wa zamani wa Burundi, Antoine Nduwayo, alifutiwa mashitaka baada ya kukutwa hana hatia kwa sababu hakuhusika na mauaji hayo.

Watu watano kati ya walioshitakiwa ambao walikuwa mahakamani, na wengine walihukumiwa licha ya kutokuwepo mahakamani.

Buyoya kwa sasa ni mwakilishi wa Umoja wa Afrika nchini Mali na ni kiongozi anayeheshimika barani Afrika pamoja na mataifa ya kigeni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...