SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum pichani kulia  na Sheikh Mohamed Iddi Mohamed (kushoto) wamejitokeza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kutangaza kufuta tofauti zao baada ya hivi karibu kuhitilafiana.

Wakizungumza wakati wa mkutano wao huo leo, Masheikh hao kwa pamoja walisema wao kama viongozi wa dini hawapo tayari kuona wanaendelea kuwa na tofauti zao kwa kuwa hata dini yao inawaelekeza hivyo.

"Sisi kama viongozi tumeona kuwa hakuna sababu ya kuendelea kuwa na uhasama katika mambo ambayo kwetu tumeona kuwa siyo busara kwetu lakini kwa waumini wetu pia" alisema Sheikh Mohamed

Alisema kwa umoja wo kama viongozi wanaoaminiwa na waumini wao, hawana sababu za kuendelea kujenga uhasama usio na tija kwa madai kuwa kufanya hivyo kungeiingiza chuki hiyo kwa waumini wao.

Aliwataka waumini wa dini hiyo na watanzania kwa ujumla kusahau kila kilichotokea na badala yake wajiandae kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano ya wiki ijayo.

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum alisema kwa sasa wao ni kitu kimoja na kwamba hakuna tena mgogoro miongoni mwao na zaidi akawataka waliokuwa wametatizwa na hali hiyo kusahau jambo hilo.

Alisema hata dini ya Kiislam imetamka wazi kwa kuwataka watu wenye tofauti ndani ya dini kuondoa tofauti zao ndani ya siku tatu na kwamba kama ambavyo wameamrishwa na dini yao wamekaa pamoja na kumaliza tofauti zao.

Aidha aliwataka waumini wa dini hiyo ambao kwa namna moja au nyingine waliingia katika mgogoro huo na kujenga utofauti kutokana na tofauti zao kufuta tofauti zao na kujiandaa na uchaguzi mkuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...