Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Dkt. Seraphia Mgembe akitoa maneno ya utangulizi wakati wa sherehe fupi za kukabidhi Hati za Hakimiliki za kimila. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya  Wilaya ya Sikonge Tito Luchagula akisoma leo taarifa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika sherehe fupi za kukabidhi hati za Hakimiliki za Kimila kwa vijiji vya  Ukondamoyo, Mole na Usanganya.Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Ukondamoyo wilayani Sikonge wakiwa katika sherehe fupi leo ya kukabidhi hati za Hakimiliki za Kimila kwa vijiji vya  Ukondamoyo, Mole na Usanganya. Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri akitoa hotuba  leo wakati sherehe fupi za kukabidhi hati ya hakimiliki ya kimila za awamu ya pili 224 kwa wanavijiji vya Vijiji vitatu na hivyo kufikisha Hati 856 ambazo zimekwishatolewa chini Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA).

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri( kushoto) akisalimiana na Meneja wa Urasimishaji Ardhi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Antony Temu(kulia) wakati apowasili leo katika Kijiji cha Ukondamoyo kwa ajili ya kukabidhi Hati za Hakimiliki za kilima.

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri (kulia) akimkabidhi leo hati ya hakimiliki ya kimila mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Ukondamoyo Johari Selemani(kushoto)  baada ya maeneo yake kuhakikiwa na kupimwa chini ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA).Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri(mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa Kijiji cha Ukondamoyo ambao maeneo yao yalihakikiwa na kupimwa na  kukabidhi hati ya hakimiliki ya kimila chini Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA).

Picha na Tiganya Vincent

********************************

NA TIGANYA VINCENT

HALMASHAURI ya Wilaya ya Sikonge imetakiwa kuhakiki na kupima mashamba ya wanavijiji ambayo hayajapimwa ili waweze kupatiwa hati ya hakimiliki ya kimila kwa ajili ya kuyaongezea thamani.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri wakati akikabidhi hati ya hakimiliki ya kimila za awamu ya pili 224 kwa Vijiji vitatu na hivyo kufikisha Hati 856 ambazo zimekwishatolewa chini Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA).

Alisema hatua hiyo itasaidia kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ambao utasaidia kuondoa migogoro miongoni mwa wanavijiji wao kwa wao.

Magiri alisema kuwa Wilaya ya Sikonge ina Vijiji 71 lakini ambavyo wakazi wamepimiwa maeneo yao ni 12 na kubaki 59, jambo ambalo linahitaji kufanyia kazi ili kukamilisha vyote.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliutaka uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanatatua tatizo la mwingiliano wa maeneo 102 katika Vijiji vya Ukondamoyo, Mole na Usanganya ambalo ulisababisha MKURABITA washindwe kuandaa hati za Hakimiliki za Kimila kwa wananchi.

Alisema sanjari na hilo ni vema wanakijiji 797 ambao hawakujitokeza wakati MKURABITA wakihakiki maeneo katika vijiji vyao wajitokeza ili nao waweze kupimiwa maeneo yao kwa ajili ya kupatiwa hati.

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Dkt. Seraphia Mgembe aliwataka wanavijiji kuhakikisha wanatumia Hati ya Hakimiliki za Kimila wanazopatiwa kuendesha kilimo na biashara zao kwa tija ili kuchangia katika maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Alisema hati hizo walizopewa ni mtaji ambao wanatakiwa kuutumia kujiongeza kipato kwa kuandaa mipango mizuri ambao itawawezesha kunufaika na fursa ya mikopo katika Taasisi za Fedha.

Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) hadi hivi sasa umesharasimisha rasilimali na biashara za wanyonge katika Wilaya 52 kwa upande wa Tanzania bara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...