*Asema hakuna mgombea yoyote wa upinzani anayeweza kushindana naye

*Dk.Magufuli ashindwa kuvumilia, asimulia yaliyomtokea Sumaye,akaondoka

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Manyara

WAZIRI Mkuu mstaafu katika Serikali ya Awamu ya Tatu Ferederick Sumaye amesema kuwa amekuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kwa miaka mitano na sasa baadae akamua kurudi Chama Cha Mapinduzi(CCM) na kwamba hakuna Chama cha kupambana na CCM kwa sasa wala anayeweza kushindana na  Dk.John Magufuli katika nafasi ya urais.

Akizungumza mbele ya Mgombea urais wa CCM na maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Manyara leo Oktoba 25,2020, Sumaye ambaye amekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, amesema kama wanavyofahamu miaka mitano iliyopita alikuwa Chadema na baadae amerudi CCM baada ya kuona kule hakuna kinachoendelea katika siasa za kuongoza nchi.

"Kiukweli hakuna Chama ambacho kinachoweza kupambana na CCM na hakuna wa kupambana na Magufuli, mimi ni mwalimu wa siasa na uongozi, huko nilikokuwa hawaaambiliki.Kwa sasa hakuna chama cha kupambana na CCM, labda kwa huko mbele safari na wala sio sasa, naomba wale wa upinzani wasipoteze muda wao, kura yao wampe Dk.John Magufuli. Sote ni mashahidi, mmewahi kumuona mgombea wao Chadema anatembea na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wao.

"Wenyewe hawako pamoja, huwezi kutoa nchi kwa mtu ambaye hawako pamoja, lazima tutoe nchi kwa watu ambao wanaweza kuongoza, ni lazima kura zote tumpe Dk.Magufuli.Watanzania wenzengu naomba niseme Dk.Magufuli ana uwezo mkubwa sana na wala hakuna sababu ya kupoteza muda wa kuhangaika na wengine Oktoa 28, tumchague Dk.Magufuli,"amesema Sumaye.

Akizungmzia Sumaye mbele ya wananchi hao, Dk.Magufuli amesema Waziri Mkuu huyo mstaafu amesema ni mwana CCM halisi ambaye alipotea katikati kutokana na mapepo yaliyomkumbuka huku akifafanua ni Waziri Mkuu aliyefanya kazi kwa Benjamin Mkapa kwa miaka 10.

"Ni Sumaye wa Mkoa wa Manyara lakini ndugu zangu wa Manyara Mungu alipoumba Malaika  wengine wakagoma, hivyo wale waliogoma walishuka duniani na kumgusa Sumaye akahama Chama, akaenda kwingine lakini amerudi mapema.Alikwenda Chama kisichokuwa na staa, chama kinachotaka watanzania tupigane wenyewe kwa wenyewe, Chama kilichoharibu yale ya baba wa taifa, wao wanachonganisha watu. Tanzania tuna dini tunaishi pamoja , Sumaye karubi nyumbani, kufanya kosa sio kosa.

"Nakumbuka hata Pauline Gekuru naye hivyo hivyo mapepo yalimkumba na hivyo akaamua kuondoa CCM lakini sasa amerudi na anafanya kazi nzuri tu.Akiwa upinzani aliona ana hubiri ambayo hayatoki moyoni, akaona yanayohubiriwa ni kama yanachochea uvunjifu wa amani.Hivyo pamoja na kupokea posho na mshahara aliamua kukihama chama hicho na kuja CCM, ni watu wachache sana wenye ujasiri wa aina hiyo, aliporudi alijeleza kwa upole na heshima kubwa,"amesema Dk.Magufuli.

Amesisitiza baada ya Gekuru kurudi CCM walimsamehe na wakamruhusu kugombea ubunge na alipogombea Babati Mjini wamempitisha ."Huyu mama ni mpambanaji, ni mtetezi wa watanzania, amepita bila kupingwa na hivyo anasubiri kuapishwa tu.

Kuhusu Mkoa wa Manyara, Dk.Magufuli amesema anaikumbuka vizuri historia ya Manyara na Babati kwani haikuwa ilivyo sasa kwani ulikuwa ni mkoa wenye shida ya miundombinu ya barabara kwani hata anakumbuka Babati ulikuwa ni mji wenye shida, haufikiki."Nakumbuka Waziri Mkuu enzi za Mkapa ndugu Sumaye tulipokuwa katika vikao vya Baraza la Mawaziri kila saa alikuwa anazungumza kuhusu barabara hiyo.

"Nakumbuka Marry Nagu alikuwa anasema mashimo ya barabarani yalikuwa na majina mengine Sumaye, mengine Nagu.Hivyo mzee Mkapa alitoa maelekezo ya kutengenezwa kwa barabara hizo, Tukajenga , nakubuka ilikuwa haiwezekani kutoka Babati kwenda Dodoma , Babati kwenda Singida ilikuwa shida.Kutoka Babati kwenda Minjingu kulikuwa kugumu, inawezeka watu wamesahau wakiwemo vijana waliozaliwa siku za hivi karibuni,"amesema Dk.Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...