Na Agness Francia, Michuzi Tv
BODI ya ligi kuu Tanzania (TPLB) imeendelea kusisitizia kuwa katika kuelekea kwa kuanza kwa ligi daraja la kwanza na la pili msimu huu wa 2020-21, viwanja vya mpira ambavyo havijakidhi viwango na matakwa ya msingi ya kikanuni, Kama yalivyoainishwa kwenye kanuni ya saba ya ligi sheria namba moja ya mpira wa miguu, inayozungumzia uwanja havitaruhusiwa kuchezewa mechi za ligi hizo.

Aidha bodi hiyo imezishauri klabu zote kuhakikisha viwanjwa vyao vinakuwa katika ubora unaohitajika ili kuweza kutumika kwa mechi zao za nyumbani.

Vile vile uongozi wa bodi ya ligi hiyo umetanabaisha kuwa haitosita kusimamisha ama kufungia uwanja wowote ule utakaobainika kutokuwa na sifa za kutumika kwa michezo ya ligi hizo.

Badala yake mechi zote za timu husika zitahamishwa katika uwanja mwingine wenye kukidhi vigezo, sifa na kwa kufuata kanuni ya saba ya ligi inayvoeleza.

TPLB imeviorodhesha viwanja vilivyotajwa na timu za ligi daraja la kwanza na la pili kwa matumizi ya mechi zao za nyumbani, navyo ni uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam utakaotumiwa na timu ya Africalyon na Transit camp FC, Mkwakwani Mkoani Tanga-Africansport FC, Nyamagana Mwanza- Alliance FC na pamba FC, Sheikh Amri Abeid Arusha-Arusha FC, Mwakangale Mbeya-Boma FC, Jamhuri Dodoma- Fountain Gate FC.

Vingine ni Nyankuru Geita-Geita gold FC, Sokoine Mbeya-Gipco FC, Ally Hassan Mwinyi Tabora -Kitayosa FC na Rhino rangers, Samora Iringa-Lipuli fc, Maji maji Ruvuma-Maji maji FC, Jamhuri Morogoro- Mawenzi markert FC, CCM kirumba Mwanza-Mbao FC, Mabatini Pwani-Mbeya kwanza fc, Nangwanda sijaona Mtwara- Ndanda FC, Sabasaba Njombe-Njombe mji FC,Pamoja na uwanja wa Liti Mkoani Singida ambao utatumiwa na timu ya Singida united FC.

Ambapo uongozi huo umemalizia kwa kusema kuwa ni matarajio yao timu zitaonyesha ushirikiano mkubwa katika jambo hilo kwa lengo la kuhakikisha ligi inachezwa kwenye mazingira rafiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...