Is-Haka Omar, Pemba

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt.
Hussein Ali Mwinyi, amesema iwapo wananchi wa Zanzibar watampa ridhaa
ya kushika nafasi hiyo, ataimarisha huduma za afya, ili wananchi
wapate uhakika wa matibabu.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika uwanja wa mpira Jimbo la Kiwani Mkoa wa kusini Pemba, kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni wa
chama hicho, uliokuwa na lengo la kuwanadi wagombea wa CCM.

Amesema, hayo ndio kipaumbele chake cha kwanza mara atapomaliza
kuapishwa, kwani mambo hayo ni miongoni mwa mambo muhimu kwa wananchi.

Amesema moja ya dhamira yake ya kugombea nafasi hiyo, ni kuwatumikia
wananchi kwa moyo wa dhati, na ndio maana anakusudia kuimrisha huduma
za afya.

Amesema atakachokifanya ni kuendeleza pale alipoishia Rais wa sasa wa
awamu ya saba, Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, ambapo anatarajia
kuimarisha miundombinu ya afya.

Dkt. Mwinyi ameahidi kuwa katika kuimarisha huduma hizo, atajenga
nyumba za kisasa za madaktari, ili wapate mahala pazuri na salama
pakufanyia kazi zao.

‘’Kama madaktari wetu wakipata nyumba za kisasa za makazi inakuwa
rahisi sana kutoa huduma za afya kwa ubora na hilo nalikusudia
kulifanya nikiwa Rais,’’aliahidi.

Aidha mgombea huyo wa urais ameahidi kuwa, dawa zitapatikana kwa
uhakika sambamba na kuajiri kwa wingi madaktari bingwa na kuimarisha maabara ili watoe huduma za tiba kwa ufanisi.

Hata hivyo Dk. Mwinyi ameahidi ujenzi wa nyumba za walimu sambamba na
kuwaendeleza kielimu, mafunzo kwa walimu ili wawe na ufanisi wa kazi
zao.

Katika hatua nyingine Mgombea huyo wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya
CCM, amesema anakusudia kuinuwa uchumi wa wazanzibari, kwa kuanzisha
viwanda mbali mbali vikiwemo vya kusarifia mwani.

Amesema, pamoja na viwanda hiyo mwani huo utaongezwa thamani kwa
kuyashawishi makampuni mengi zaidi  kununua mwani wa wakulima wa
Zanzibar.

“Kilio cha wakulima wa mwani na wavuvi nimeshaskia wakati nakutana na
makundi mbali mbali kwenye kampeni zangu, sasa nikichaguliwa kuwa
Rais, nitahakikisha naimarisha sekta hiyo." amesema.

Katika eneo jingine Dk. Mwinyi amesema mafanikio ya Zanzibar
yanategemea sana utendaji kazi wa kila mmoja, hivyo suala la
uwajibikaji ni jambo la lazima.

Amesema kuwa, serikali atakayoiongoza hatopenda hata kidogo kuona
ndani yake kuna watendaji wasiopenda kuwajibika, kwani wanakuwa
kikwazo kufikia maendeleo yaliokusudiwa.

Ameeleza, jambo hilo ni adui mkubwa wakufikia maendeleo ya  Zanzibar,
na kuendelea kudumaa kwa baadhi ya sekta, jambo ambalo halikubaliki na
atalisimamia kwa dhati.

“Mkinichagua kuwa Rais wa Zanzibar, pamoja na mambo kadhaa ambayo
ntawafanyia, lakini suala la uwajibikaji ndio kipaumbele cha kwanza,
na akitokezea mtendaji kushindwa kuwajibika, nitamuwajibisha.’’ameeleza.

Mapema Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.
Ali Mohamed Shein, amesema CCM imewaletea kiongozi mchapakazi kwa
wananchi wa Zanzibar.

Amesema sifa za Dkt. Mwinyi za nidhamu, uhodari wa kazi, kuwajali watu
wote na ubobevu wa uongozi, hakuna mgombea mwengine yeyote kwa nafasi
yoyote kutoka vyama upinzani.

Ameeleza kuwa, Dkt. Mwinyi amekuwa anajali sana shida za watu na
kupelekea kushika nafasi mbali mbali, kuanzia serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...