NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza limewapongeza wadau wa uchaguzi mkoani humu kwa kufanya uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu.   

Muliro alitoa kauli hiyo jan wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi mkuu uliofnyika Oktoba 28, mwaka huu.

Alisema katika Mkoa wa Mwanza,jeshi l polisi liliimarisha usalama kwa kiwango cha juu na kuufanya uchaguzi mkuu wa mwaka huu,kufanyika kwa haki, uhuru,amani na utulivu bila bughudha.

“Jeshi la polisi linawapongeza wadau wa uchaguzi ambo walitoa taarifa mbalimbali za watu waliokuwa wakipanga njama za kufanya vurugu na fujo ambo walikamatwa na kuhojiwa baadaye kuachiwa kwa dhamana na kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kwa amani,hakuna matukio makubwa ya ajabu ya kuathiri mchakato wa uchaguzi mkuu,”alisema Muliro.

Alisema jeshi hilo linafuatilia kwa karibu mchakato wote wa uchaguzi mkuu 2020, kabla, wakati na baada ya kupiga kura katika wilaya na majimb
o yote na zipo taarifa za vikundi ama watu kupanga kufanya vurugu.

Muliro alisema wanaendelea kufuatilia mienendo ya taarifa za watu wanaodaiwa bado wana mipango ya kutaka kufanya fujo au vitendo vya kihalifu.

Alieleza kuwa jeshi hilo halitamvumilia mtu yeyote ama kikundi chochote kitakachobainika kuandaa mipango ya kufanya vitendo vyovyte vinavyokinzana na sheria za nchi.

“Polisi hawataruhusu kundi la watu kula njama za kufanya fujo baada ya matokeo yote ya uchaguzi kutangazwa, watakaothubutu watajiingiza kwenye mgogoro na msuguano na jeshi la polisi, hatutakubali watu kuingia barabarani na hatutamvumilia yeyote na atakayethubutu kupanga njama hizo za vurugu,”alisema Muliro.

Aliwataka wananchi mkoani Mwanza kuwa watulivu na kufanya shughuli zao za uzalishaji na kiuchumi kwa uhuru kwa sababu jeshi la polisi liko mitaani na limeimrisha usalama kwa kiwango cha juu kuhakikisha amani na utulivu unakuwepo muda wote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...