Na Amiri kilagalila,Njombe

Siku chache baada ya katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania Sheikh Issa Ponda kutoa kauli kuwa waislamu wote nchini wamekubaliana kumchagua mgombea wa Urais  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu.viongozi wa dini mkoa wa Njombe wakiongozwa na Sheikh wa mkoa Rajabu Msigwa wamewataka watanzania kupuuza kauli hiyo kwa kuwa sio msimamo wa waslamu
Wakizungumza na vyombo vya habari mjini hapa Sheikh wa mkoa  Rajabu Msigwa na Sheikh wa wilaya ya Njombe Shabani Dinga Dinga wamesema.


"Kauli ile si kauli sahihi na ni kauli ya upotoshaji kwa kuwa sisi kama waislamu jambo hilo lingeelezwa na mkuu wetu wa taasisi"alisema Sheikh Rajabu Msigwa 

Sheikh wa wilaya ya Njombe Shabani Dinga Dinga amesema"Hakuna kikoa cha namna hiyo maneno haya kwanza ningependa kusema myapuuze,baraza kuu la waislamu Tanzania Bakwata lina mfumo ambao kiongozi mkubwa katika nchi hii ni Mufti shegh mkuu wa Tanzania na ndie msemaji wa waislamu wote bila kuzingatia taasisi ya aiana yoypte iliyopo chini yake.Maneno hayo tuyapuuze"alisema Shabani Dinga Dinga Sheikh wa wilaya ya Njombe 

Kauli hiyo pia imeibua hisia kwa wachungaji wa dini ya kikristu ambao wanasema inaweza kuwagawa watanzania.

"Mh, Tundu Lissu ilitakiwa naye akanushe maneno ya mtu kwamba mimi naomba kura za watanzania wote na watanzania tuna wakristo na waisalamu"alisema Mchungaji Tweve wa kanisa la TAG Melinze mjini Njombe


"Ninawasihi wakristo kwa waslamu wapuuze kauli kama hii lakini pia kiongozi wa Chama husika najua ana uwezo mkubwa wa kielimu akanushe kauli hiyo kwasababu ni kinyume cha katiba ya Tanzania"alisema mmoja wa wachungaji wa kanisa la KKKT mjini Njombe


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...