Na Shukrani Kawogo, Njombe.

Wakazi wa kata ya Lumbila wilayani Ludewa mkoani Njombe wamemuomba mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kuwaboreshea bandari ambayo imekufa kwa miaka mingi.

Maombi hayo wameyatoa wakati wa mkutano uliofanywa na mbunge huyo katika kijiji cha Lumbila kata ya Lumbila.

Akizungumza kwa niaba ya vijana wanaoishi katika kata hiyo Frank Lukuwi amesema vijana wengi wa kata hiyo wanategemea uvuvi hivyo kukosekana kwa bandari hiyo kunawafanya washindwe kukua kiuchumi.

Alisema wanamshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuwaletea meli lakini zimekuwa zikipita kwa mbali.

"Tunamshukuru Rais Magufuli katuletea meli lakini tunaomba vituo viongezwe vya kusimama meli ili nasisi tuweze kunufaika", Alisema Lukuwi.

Aidha kwa upande wa mbunge mteule Joseph Kamonga amesema Rais Magufuli ameonyesha dhamira ya dhati katika kuboresha bandari zilizokufa ambapo kwa Sasa ameanza na bandari ya Lupingu na Manda.

Aliongeza kuwa sambamba na hilo mamlaka ya bandari bado inaendelea kufanya utafiti juu ya maeneo ya kuweka vituo hivyo.

" Mamlaka ya bandari tayari imeanza kufanya tafiti juu ya maeneo ya kuweka vituo hivyo msiwe na wasiwasi vituo vitakuwepo vya kutosha", Alisema Kamonga.

Alisema kuongezeka kwa vituo hivyo kutapelekea wananchi wanaoishi kando kando ya ziwa nyasa kufanya biashara na kupata urahisi wa kusafirisha bidhaa zao.

Aliongeza kuwa wananchi wengi wa ukanda wa mwambao wananunua bidhaa mbalimbali kutoka Mbeya na kusafirisha kwa gharama kubwa hivyo uwepo wa meli qhizo utawasaidia kusafirisha kwa gharama ndogo zaidi.

Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akisalimiana na wananchi alipowasili eneo lamkutano wa kumuombea kura rais John Pombe Magufuli.
Vijana walio ongozana na mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kwenda kumuombea kura rais John Pombe Magufuli wakiburudika ndani ya boti walipokuwa wakielekea vijiji mbalimbali vilivyopo kandokando ya ziwa nyasa.
Wakazi wa Kijiji cha Kirondo kata ya Kirondo wakiwa wamembeba mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kumpeleka katika eneo la mkutano baada ya kumshusha kutoka Mwenye boti.
Vijana wa Kijiji Cha Kirondo kata ya Kirondo wakimshusha Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kwenye boti alipowasili kufanya mkutano katika kijiji hicho akitokea Kijiji Cha Lumbila.
Wananchi wa Kijiji Cha Kirondo wakiwa kandokando ya ziwa nyasa wakimsubiri kumpokea mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (Aliyevaa boya la kuogelea) akiwa kwenye boti pamoja na timu yake wakitembelea vijiji mbambali vilivyopo kandokando ya ziwa nyasa kwa lengo la kumuombea kura rais John Pombe Magufuli.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kulia) akimsikiliza kijana mkazi wa kata ya Lumbila Frank Lukuwi wakati akieleza uhitaji wao wa kuongezwa vituo vya meli.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akijiandaa kushuka kwenye boti baada ya kuwasili kijiji anachotakiwa kufanya mkutano.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (Mwenye t-shirt ya kijani)akiwa amejifunga kikoi akicheza ngoma ya kihoda alipokuwa kwenye mkutano wa kumuombea kura rais John Pombe Magufuli.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kirondo alipokuwa kwenye mkutano wa kumuombea kura rais John Pombe Magufuli katika Kijiji hicho.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...