Mhandisi John Chacha Nyamuhanga Mratibu Umwagiliaji wa Mradi wa Regrow akiongelea kuhusu lengo la Mradi katika Skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji ya Isinyela, Iliyopo Chimala Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.

Katika picha ni sehemu ya Miundombu ya asili ya Umwagilaiji inayotumika na wakulima katika skimu ya Isenyela Wilayani Mbarali. Mradi wa Regrow unategemea kufanya maboresho ya miundombinu hiyo.
Mkulima wa zao la Mpunga Bw. Rahim Mbule, akiongelea kuhusu faida zaidi anazotegemea kupata baada ya maboresho ya miundombinu ya uwagiliaji.

Na MwandishiWetu; Mbarali

WAKULIMA wilaya ya Mbarali katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Makangalawe na Isenyela wamepatiwa elimu kuhusu Uimarishaji wa chama cha wamwagiliaji juu ya usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi ya maji ya umwagiliaji kupitia mradi wa Regrow unaolenga kukuza utalii kusini mwa Tanzania na kukuza shughuli mbadala za kiuchumi zitakazoleta matokeo katika utunzaji wa maliasili na rasilimali maji.


Akizungumza katika mafunzo hayo mratibu wakiufundi wa mradi huo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi, John Chacha Nyamhanga alisema kuwa,wakulima hao wanatakiwa kuelewa namna sahihi ya matumizi ya maji katika kilimo hicho ili kusiwepo na upotevu na upungufu wa maji katika mto Ruaha Mkuu unaotegemewa zaidi na hifadhi za Taifa za Ruaha na Mwalimu Nyerere usimamizi bora wa rasilimali maji utapelekea pia upatikanaji maji na uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na vyanzo vya maji.


Sambamba na hilo Mhandisi Nyamhanga aliongeza kwa kusemakuwa, lengo kuu la mradi nikuwawezesha wakulima kulinda vyanzo vya maji na kuboresha miundombinu ya umwagiliaji ili kuweza kuongeza tija naongezeko la maji katika mto Ruaha mkuu kwa ajili ya matumizi ya wanyamapori ili kuweza kukuza utalii katika ukanda wa kusini na shughuli mbadala za wanchi.


“Mradi Umejikita zaidi katika kuboresha Miundombinu ya umwagiliaji kwa maana yakuboresha mabanio ili kuwezesha usimamizi wa maji na  kuhakikisha kwamba wakati wa kiangazi kuna  upatikanaji wa maji ndani ya mito yote ambayo ipo juu ya ardhi OevuyaIhefu inayokusanya maji kwa ajili ya mto Ruaha Mkuu. Alisisitiza.


Kwa Upande wake Mhandisi wa Umwagiliaji wa Wilaya ya Mbarali Bw.Karoli Lihala, alisema kupitia mradi huo Miundombinu ya Umwagiliaji itaboreshwa katika maana ya kusakafiwa pamoja na mifereji mingine ya kugawa na maji ndani ya skimu.


Awali,akiongea katika Mafunzo hayo mkulima katika skimu ya umwagiliaji ya Isenyela Bw. Rahim Mbule, alisema ana mategemeo ya kupata mafanikio zaidi kupitia kilimo cha umwagiliaji baada ya maboresho ya miondombinu.


Mradi huo wa Regrow unaotekelezwa na Serikaliya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Wizara ya Maliasili na utalii, unalenga kuongeza utalii kusini mwa Tanzania katika hifadhi za taifa za Ruaha, Udzungwa, Mikumi na Mwalimu Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...