Na Jane Edward Michuzi TV,Arusha
Wanachama wa chama cha kuweka na kukopa cha Ngome Saccos wametakiwa kuendelea kuwa na imani na chama hicho huku wakiendelea kujijengea uwezo zaidi wa kuweka akiba.
Hayo yalisemwa jana mjini hapa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho,Brigedia Generali Omari Matteka wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na chama hicho.
Brigedia Generali Matteka alisema kuwa, chama hicho kilisajiliwa rasmi mwaka 2007 na ni kati ya vyama vya kuweka na kukopa kongwe vilivyopo jijini Dar es Salaam .
Aliongeza kuwa ,wanachama wa chama hicho ni wanajeshi ,watumishi wa umma na wale waliostaafu katika wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa ambapo wana jumla ya wanachama 13,000 nchi nzima.
Brigedia Generali alisema kuwa ,wana programu maalumu ya kuwaandaa wastaafu ambapo hutoa mkopo kwao miezi sita kabla pindi anapokaribia kustaafu ili kufanya maandalizi mapema .
"kwa kweli Saccos yetu tangu tumeanzisha tumeweza kuwakopesha wanachama wengi sana ambao wameona manufaa na matunda makubwa ya sacoss hii,na wameweza kuanzisha miradi mbalimbali "alisema Brigedia Generali.
Aliongeza kuwa,kwa mwezi wamekuwa wakikopesha wanachama wake wastani wa shs 3.8 bilioni.
Alifafanua zaidi kuwa,wanachama wengi wameweza kufaidika na kuanzisha makazi Bora pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo jambo ambalo limeleta mafanikiwa makubwa kwao.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi mbalimbali kuzitumia vizuri vyama hivyo vya kuweka na kukopa kwani ni mwarobaini wa kutatua changamoto mbalimbali sambamba na kuweza kuanzisha miradi .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...