Na Woinde Shizza ,ARUSHA


MKUU wa Mkoa wa Arusha Iddi kimanta amewakabidhi wazee zaidi ya 6000 bima za CHF ambazo zitawawezesha kupata huduma za matibabu.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kadi hizo Kimanta amesema kwamba  kadi hizo zitawapunguzia  unafuu wa maisha na kuwasaidia wazee hao kutibiwa kwa urais bila garama yeyote.

Amesema Jiji la Arusha limefanya jambo la muhimu la kuwathamini wazee kwa kuwapatia kadi hizo za matibabu zitakazowawezesha wazee kupata huduma za kiafya,pindi wanapokuwa wanaumwa.

"Unajua mzee ana garantini ya kuumwa saa yoyote anaumwa hivyo kwa kupata kadi hii utawasaidia Sana kupunguza gharama za matibabu yao ,unaeza kuta mzee anatumia ata laki nne kwa mwezi kwa ajili ya kujitibu,"amebainisha Kimanta

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Rebeka Mongi amesema Jiji hilo limetenga jumla ya Sh.milioni 41 kwa mwaka wa fedha 2020/2012 kwa ajili ya kuwalipia  wazee bima za afya.

Wakati huo huo Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dk.Kheri Kagya amesema waliona changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee ndio maana wakaamua kuwajali na kuwapatia bima ya afya ambayo utawasaidia kutibiwa hadi katika hospital za rufaa.

Awalo akisoma risala kwa Mkuu wa Mkoa Katibu wa Baraza la Wazee Jiji la Arusha ,Kasimu Seramu ametaja baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo ni pamoja na ukosefu wa madaktari maalum kwa ajili ya kuwahidumia wazee na kubainisha kuwa japo mahospitali mengi yana madirisha ya wazee lakini wauguzi kwaaji ya wazee hawana

Aidha changamoto nyingine inayowakabili ni pamoja na ukosefu wa dawa kwa ajili ya magonjwa yasiyoambukiza ,yanayowakumba wazee,pamoja na okosefu wa uwakilishi Katika Taasisi za juu na kwamba kwa sasa wameanza kujipanga kwa ajili ya kuunda baraza la wazee la taifa ambapo wanatarajia kufanya uchaguzi Wao Novembe 15 ambapo watapata viongozi wakuwasemea kitaifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...