Jumla ya Wapiga Kura 29,754,699 wanatarajiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao unaotarajia kufanyika hapo kesho.

Ambapo Wapiga Kura wapatao 29,188,348 wameandikishwa katika Daftari ya kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), na Wapiga Kura 566,352 wameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ( ZEC ).

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage amesema kuwa katika Uchaguzi huu, Tume itatumia jumla ya vituo vya Kupigia Kura 81,567 vikiwemo vituo 80,155 vinavyotokana na Daftari la Kuduma la Wapiga Kura NEC na vituo 1,412 vinavyotokana na Daftari la Wapiga Kura la ZEC.

Aidha Jaji Kaijage amesema vyama vyote 19 vyenye usajili wa kudumu vinashiriki uchaguzi huu kwa kusimamisha wagombea katika nafasi mbalimbali za uongozi.

" Kwa mujibu wa takwimu kuna jumla ya wagombea 1,257 katika nafasi ya Ubunge na kuna jumla ya wagombea 9,237 katika nafasi ya Udiwani". Amesema Jaji Kaijage.

Jaji Kaijage amesema vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni.

" Ifikapo saa 10:00 jioni mlinzi wa kituo atasimama nyuma ya mpiga kura wa mwisho kwenye mstari ili kuhakikisha kwamba mpiga kura anayepiga kura ni yule aliyefika ndani ya muda uliobainishwa". Amesema Jaji Kaijage.

Pamoja na hayo Jaji Kaijage amesema mpiga kura anatakiwa kuwatambua na kutoa kipaumbele kwa watu wenye mahitaji maalumu kama vile wazee, wagonjwa, watu wenye ulemavu, wajawazito na akina mama wanaonyonyesha bao watakwenda vituoni na watoto.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage akizungumza mbele ya Waanishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar,alipokuwa akitoa neno la Mwisho kwa Watanzania kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hapo kesho Oktoba 28,2020 nchi nzima.Jaji Kaijage alisema kuwa katika Uchaguzi huo, Tume itatumia jumla ya vituo vya Kupigia Kura 81,567 vikiwemo vituo 80,155 vinavyotokana na Daftari la Kuduma la Wapiga Kura NEC na vituo 1,412 vinavyotokana na Daftari la Wapiga Kura la ZEC,ambapo Jumla ya Wapiga Kura 29,754,699 wanatarajiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu
Sehemu ya meza kuu ya mkutano huo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...