Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza katika Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekemea vitendo vya kupigwa kwa Wanawake na Watoto wa kike vinavyotokea katika Jamii.
 
Dkt. Tulia ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kampeni ya Siku 16 za kupinga Ukatili zikiongozwa na Kauli mbiu isemayo: "Tupinge vitendo vya Ukatili: Mabadiliko yananza na mimi."
 
Dkt. Tulia amesema kuwa Jamii inatakiwa kuanza kutambua mchango wao katika juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya vitendo vya Ukatili vinavyotokea katika jamii.
 
"Jamii tuchukue hatua zaidi haya yanayotokea katika Jamii tunaweza tukayaponga na kuyakataa ndio maana tunasema mabadiliko yananza na mimi." amesema.
 
Aidha amesema Serikali imekusudia kuendelea kushirikiana na Mashirika ya Kimataifa na Kitaifa ili kuhakikisha vitendo vya Ukatili katika jamii vinatokomezwa nankutoweka katika Jamii.
 
Pia Dkt. Tulia ameitaka jamii kuwapa fursa watoto wa kike sawa na watoto wa kike katika nyanja mbalimbali hasa katika kupata elimu na kusisitiza Jamii kuwaheshimu Wanawake na Watoto wa kike.
 
Akizungumzia utekekezaji wa Mipango mbalimbali ya Kutokomeza Vitendo vya Ukatili Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kuhakikisha vitendo vya ukatiki dhidi ya wanawake na Watoto vinatokomezwa nchini.
 
"Tutaendelea kutilia mkazo suala hili kwa nguvu zaidi na kutafuta namna mbalimbali za Mapambano ya Kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto" amesema.
 
Naye Mkurugenzi wa Wildaf Anna Kulaya amesema kuwa Wanawake wa vijijini na hasa wenye elimu duni wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kikatili hivyo jitihada kubwa zinahitajika katika kuhakikisha Jamii hiyo unapata elimu ya kutokomeza vitendo vya kikatili.
 
"Utashangaa sana hata katika Vyuo na Vyuo vikuu kumekuwa na taarifa nyingi za uwepo wa vitendo vya kikatili kwa wanafunzi katika Vyuo hasa uwepo wa rushwa ya ngono." amesisitiza.
 
Wakati huo huo Mhe. Tulia Ackson alizindua GBV APP maalum kwa ajili ya wananchi kutoa na kupata taarifa mbalimbali kuhusu vitendo vya ukatili ikiwemo elimu juu ya mapambano dhidi ya vitendo hivyo.
 

Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akizindua GBV APP kwa ajili ya kupata taarifa za Ukatili wa Kijinsia wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam kulia mwenye koti  ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya - Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya - Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea utekelezaji wa Afua mbalimbali za Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akiangalia muonekano wa GBV APP iliyotengenezwa kwa ajili ya kupata taarifa za Ukatili wa Kijinsia wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam kulia mwenye koti ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya - Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja pamoja na wanaharakati wa Mapambano dhidi ya Ukatili wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto jijini Dar es Salaam wa pili kushoto waliokaa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...