MFANYABIASHARA Ayubu Kiboko na mke wake Pilly Mohammed Kiboko wanaotuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa gramu 251.25 aina ya heroin wamepatikana na kesi ya kujibu na sasa wanatakiwa kuanza kujitetea.

Uamuzi huo umetolewa leo Novemba 27, 2020 na mahakama Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu Mahakama ya Mafisadi, jijini Dar es Salaam, baada ya upande wa mashtaka kufunga kesi yao kwa kuwaita mashahidi sita na vielelezo 16 yakiwemo magari matatu Toyota Prado, Toyota Hilux na Toyota  Land Cruiser.

Akisoma uamuzi huo Jaji Lilian Mashaka aliyekuwa akimsikiliza kesi hiyo amesema, upande wa mashtaka  umefunga kesi yao na Mahakama imefunga kwa upande wa mashtaka.

"Upande wa mashtaka kupitia mashahidi wao sita na vielelezo hivyo, wamaweza kuthibitisha kuwa kuna kosa washtakiwa mmetenda, hivyo mahakama imeona mnayo kesi ya kujibu lakini mna haki ya kutoa utetezi wenu chini ya kiapo na pia mnahaki ya kuleta mashahidi wenu, amesema Jaji Mashaka

Hata hivyo washtakiwa walipoulizwa watajitetetea kwa njia gani,  mshtakiwa wa pili (Pilly) akaanza kuangua kilio lakini  jaji alimtaka asilie bali ajipange kuja kutoa utetezi wake.

" Nakuomba usilie, hapa mmekuja kutafuta haki, unatakiwa ujipange uje ujitetee, ukilia sasa hivi haitasaidia, jipange utoe utetezi wako,"akasema Jaji Mashaka 

Washtakiwa wamedai kuwa watajitetea kwa kiapo, ambapo Wakili wao, Majura Magafu amedai kuwa hawana cha kuongeza, lakini siku ya utetezi wao wataleta kadi za magari halisi.

Aidha, Wakili wa Serikali, Salim Msemo aliiomba Mahakama hiyo kama itaridhia gari hizo ziwe chini ya Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kulevya (DCEA) kutokana na hali ya magari hayo, ambapo Jaji alitaka jina la  mtu ambae atayahifadhi hayo magari na sio ofisi.

"Nina mkabidhi Inspekta Hassan Msangi kielelezo P13, P14 na P15 kwa ajili ya kuhifadhi na anapaswa kuyaleta jumatatu,  Novemba 3, Washtakiwa mtaendelea kuwa nchini ya uangalizi, mjiandae mje kutoa utetezi wenu," amesema 

Shahidi wa mwisho kwa upande wa mashtaka katika kesi hiyo Raymond Kimambo ambaye ni jirani yake Kiboko, aliieleza Mahakama jinsi alivyoshuhudia upekuzi nyumbani kwa mfanyabiashara huyo.

Mbali na wakili Msemo, mawakili wengine wa Serikali wanaoendesha kesi hiyo, Costantine Kakula na Candid Nasua.

Katika kesi ya uhujumu uchumi namba 29/2018, Kiboko na mkewe wanadaiwa, Mei 23, 2018 eneo la Tegeta Nyuki Masaiti wilaya ya Kinondoni,  walisafirisha dawa za kuÄşevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu251.25.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...