....wateja watano wengine wazawadiwa shilingi milioni 1 kila mmoja.


Mkuu wa Kitengo cha Masoko Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella (katikati ) akichezesha droo ya promosheni ya Vodacom Shangwe Shangwena iliyochezwa leo ambapo zawadi ya kwanza ya gari aina ya Renault KWID imekwenda kwa Happyness Manembe Appolo mwenye umri wa miaka 46 mkazi wa Biharamulo mkoani Kagera. Jumla ya magari matano, pesa taslimu shilingi milioni 25 na zawadi kemkem zenye thamani ya zaidi ya shilingi 3 bilioni kutolewa ndani ya wiki 5. Kuongeza nafasi ya ushindi fanya miamala ya M-Pesa kadri uwezavyo msimu huu wa sikukuu. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu na Mwakilishi toka Bodi ya michezo ya kubahatisha, Rasul Masoud
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu akiongea na mmoja kati ya washindi waliojishindia kitita cha shilingi milioni moja wakati wa kutangaza washindi waliojishindia bahati nasibu ya promosheni ya Vodacom Shangwe Shangwena iliyochezwa leo ambapo watumiaji watano wa Vodacom M-PESA wamejishindia pesa taslimu shilingi milioni moja na mmoja wao bi Happyness Manembe Appolo kutoka wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kujishindia Gari aina ya Renault KWID. Jumla ya magari matano, pesa taslimu shilingi milioni 25 na zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi 3 bilioni kutolewa ndani ya wiki 5. Kuongeza nafasi ya ushindi fanya miamala ya M-Pesa kadri uwezavyo msimu huu wa sikukuu.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...