MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa kesho Novemba 24,2020 kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani(Ikijumlisha  visiwa vya Mafia) na Lindi.

Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Novemba 23, 2020 ya Utabiri wa siku tano  imesema mvua hiyo ya kesho inaweza kusababisha athari mbali mbali ikiwa ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi huku ikisisitiza wananchi kuzingatia agizo hilo pamoja na kujiandaa.

Hata hivyo, TMA katika taarifa yake hiyo umesema, hali ya hewa kwa siku tano kuanzia Novemba 23 imeonesha kuwepo kwa hali ya kawaida ya hewa kwa siku nyingine isipokuwa kesho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...