Mkuu wa Mkoa wa Mwaza Bw John Mongella (kushoto) akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Muwakilishi ya Makampuni ya Bakhresa Bw Leonce Josephat ikiwa ni kutambua mchango wa kampuni hiyo kwenye mbio hizo ambapo kampuni hiyo ilitoa maji yake chapa ya Uhai kwa ajili ya washiriki wa mbio hizo.


Mkuu wa Mkoa wa Mwaza Bw John Mongella (katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mbio za Rock City Marathon kutoka Kampuni ya Uhandisi ya Magare ya jijini Mwanza sambamba na washiriki kutoka kituo cha watoto wenye uhitaji maalum cha Tunaweza ambacho kinafadhiliwa na kampuni hiyo.



Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta TIPER, Bw Emmanuel Kondi (Kulia) akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za km 21 za Rock City Marathon mwanariadha kutoka Kenya Edward Kibet (Katikati) alietumia muda 1:04:52 kumaliza mbio hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza. Wengine ni washindi wa pili na wa tatu wa mbio hizo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magare, Mabula Magangila akionesha tuzo baada ya washiriki kutoka kampuni hiyo kuibuka washindi wa kwanza kwenye mbio za Rock City Marathon kwa upande wa mashirika. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwaza Bw John Mongella (Kushoto).

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongela (alievaa kofia) akishiriki kwenye mbio za Rock City Marathon zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza. Mh Mongella alifanikiwa kumaliza mbio za km 10.

Matukio mbalimbali katika mbio hizo.








 

Wakati msimu wa  11 wa mbio za Rock City Marathon ukihitimishwa kwa washiriki kutoka nchini Kenya kutamba kwenye mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella amesema ushiriki wa idadi kubwa ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi kumekuwa na faida kubwa kiuchumi katika mkoa huo.

Rock City Marathon msimu wa 11 zilihusisha mbio za km 21, km 10 na Km 5 ambapo washiriki takribani 3000 kutoka ndani na nje ya nchi walishiriki zikiwemo klabu za wakimbiaji kutoka mikoa mbalimbali, mashirika na taasisi, viongozi wa serikali, watu wenye ualbino na watoto zinatajwa kuwa ni miongoni mwa mbio kubwa nchini zikiwa na lengo la kukuza vipaji wa mchezo huo sambamba na kutangaza utalii wa ndani hususani kanda ya Ziwa.

Katika mbio za km 21 upande wa wanaume ilishuhudiwa mwanariadha kutoka Kenya Edward Kibet akiibuka mshindi wa kwanza akitumia muda wa 1:04:52 akifuatia Mkenya mwenzie Bernard Msau alietumia muda wa 1:04:55 huku nafasi ya tatu ikishikwas na Mtanzania Mathayo Sombi alietumia muda wa  1:06:11.

Kwa upande wa wanawake pia ilishuhudiwa mwanariadha kutoka Uganda Doreen Chemuthi akiibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 1:15:06, akifuatiwa na Mkenya Nesphine Teplenting alietumia muda wa 1:15:35, huku pia mshindi wa tatu akishikiliwa na Mkenya Cecilia Wayda alietumia muda wa 1:15:49.

Katika mbio hizo za wanawake nafasi ya pili hadi ya tisa zilishikiliwa na wanariadha kutoka Kenya huku Mtanzania Angelina Tsere akifanikiwa kushika nafasi ya kumi kwa kutumia muda 1:26:56 akifutiwa na Mtanzania mwingine Sara Hhiiti alitumia muda 1:26:56

Katika mbio hizo ilishuhudiwa mwanariadha wa Kimataifa kutoka Tanzania Alphone Simbu akishindwa kutamba kwa kile alichoeleza kuwa ushiriki wake kwenye mbio hizo ni mwanzo wa kujiandaa ili aweze kufanya vizuri kwenye mbio za kimataifa baada ya kutofanya mazoezi kwa muda mrefu kutoka na kusumbuliwa na majeruhi.

Akizungumza wakati wa kilele cha mbio hizo zilizofanyika kwenye viunga vya jengo la Biashara la Rock City Mall, jijini Mwanza RC Mongella alionyesha kuridhishwa na kasi ya ukuaji wa mbio hizo akibainisha kuwa ongezeko la washiriki katika mbio hizo limekuwa likileta tija katika uchumi wa mkoa huo sambamba na kutangaza utalii wa Kanda za Ziwa.

“Ukuaji huu unaoshuhudiwa katika mbio hizi ishara tosha kuwa zitakuwa ni moja yam bio kubwa sana si tu hapa nchini bali pia kimataifa. Naamini tutaendelea kupokea wageni wengi zaidi wakiwemo watalii watakaokuja pia kutembelea vivutio vya utalii tulivyo navyo Kanda ya Ziwa,’’ alisema.

Zaidi aliwapongeza wadau mbalimbali walioshiriki kufanikisha mbio hizo wakiwemo Chuo Kikuu cha MtakatifuAugustino (SAUT) cha  Mwanza, kampuni za TIPER, Magare Company Ltd, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), KCB Bank, Kampuni ya Ulinzi ya Garda World, CF Hospital, Bugando Hospital, Azam Bakhresa Group kupitia maji ya Uhai, Pepsi, Vituo vya TV vya Azam na ITV pamoja na vyombo vyote vya habari kwa kuzitangaza vyema mbio hizo.

 Akizungumzia matokeo hayo Mshauri wa Masuala ya Ufundi wa Mbio hizo Bw John Bayo pamoja na kuwapongeza wanariadha kutoka Kenya kwa kufanya vizuri alisema kuwa  Tanzania haikupata ushiriki wa wanariadha wengi wa kutokana na wengi wao kuangalia zaidi mbio za kimataifa na hivyo kutoa mwanya kwa wanariadha hususani wa Kenya kuweza kutamba kwenye mbio hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...