Dickson Tarimo Diwani wa Kata ya Makuyuni jimbo la Vunjo aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Halmashauri ya Moshi akisaini matokeo ya kukiri ameshindwa.
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Moshi DC walipokutana kumpongeza aliyeshinda uwenyekiti wa halmashauri hiyo Diwani wa Kata ya Okaoni Morris Makoi.


MADIWANI wa halmashauri ya Moshi  DC mkoani Kilimanjaro, wamemchagua Diwani wa Kata ya Okaoni Morris Makoi kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kishindo.

Uchaguzi huo uliofanyika  mwanzoni mwa wiki hii, walimchagua Makoi kuwa mshindi kwa kura  30 huku kura 16 zikienda kwa mpinzaniwake Dickson Tarimo Diwani wa Kata ya Makuyuni Jimbo la Vunjo.

Halmashauri hiyo ina wajumbe wa baraza la madiwani 48, madiwani 43,  wabunge watano, madiwani viti maalumu 11 na madiwani wa kata 32 hata hivyo wajumbe wawili hawakupiga kura huku Mbunge mmoja wa vitimaalum Shaly Raymond hakuhudhuria na diwani wa Kata ya Kibosho Kati hakupiga kura kwa kuwa kata yake uchaguzi uliahirishwa. 

Uchaguzi huo ulianza mapema majira ya saa nne asubuhi wajumbe walianza kufika ukumbini na kuketi, majira ya saa tano msimamizi wa uchaguzi ambaye ni katibu wa wilaya hiyo Miriam Kaaya alitoa maelekezo ya uchaguzi na kutaja majina ya wagombea nafasi ya Mwenyekiti kuwa ni watatu yaliyorudishwa na kamati kuu kati ya kumi na tatu waliyochukua fomu ambayo ni, Morris Makoi Diwani wa Ukaoni, Alli Badi Diwani wa Kimochi na Dickson Tarimo Diwani  wa Makuyuni.

Wajumbe kwapamoja wakamchagua Diwani wa Kata ya Uru Kusini Wilydadi Kitaly kuwa mwenyekiti wa muda,zoezi la kupiga kura lilifanyika kwa utulivu mkubwa sana huku kila mjumbe akiwa na utulivu. 

Baada ya zoezi la kuhesabu kura Msimamizi wa uchaguzi alitoa nafasi kwa wagombea kuzungumzia namna uchaguzi ulivyofanyika.

Dickson Tarimo alisema "ukweli ni kwamba uchaguzi umefanyika kwa usawa na  mimi bado mdogo nashukuru Mungu hata kwa hatua hii naamini nitafanya vizuri kipindi kijacho."alisema Tarimo.

Tarimo aliongeza kuwa, "uchaguzi huu nimejifunza mengi hasa kuhusu Demokrasia iliyotumiaka kwani kamati yangu ya siasa ya wilaya imefanya imeonyesha demokrasia ya hali ya juu katika uchaguzi huu wa ndani, na ninahaidi kushirikiana na mwenyekiti wetu aliyepitishwa leo Makoi katika kumsaidia Raisi Magufuli kuwatumikia wananchi."alisema Tarimo. 

Alibadi alisema "uchaguzi ulikuwa wa haki na uwazi lakini nachojua katika maisha ya siasa kunakuwa na makundi niwaase waheshimiwa madiwani tuvunje makundi tujenge Halmashauri ya Moshi." alisema Badi.

Kwa upande wake Morris Makoi ambaye ameshinda nafasi hiyo alisema,

 ''Uchaguzi umefanyika kwa uwazi kabisa niwapongeze kamati ya siasa ya wilaya yetu kwa kusimamia mchakato vizuri sana, nataka niwaombe wabunge twende tukachape kazi tukamilishe haadi za mh Rais Dkt..Magufuli ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa Halmashauri Mpya ya wilaya ya Vunjo."alisema Makoi. 

Baada ya wagombea wote kuzungumza msimamizi wa uchaguzi alitangaza matokeo ya kura zilizopigwa  na kutangaza mshindi. 

"Kura zilizopigwa ni arobaini na sita hakuna kura iliyoaribika, na matoke ni ifutayo Ali badi amepata kura 0, Dickson Tarimo amepata kura 16 na Morris Makoi amepata kura 30".

"Kwa mamlaka niliyopewa namtangaza Morris Makoi kuwa mwenyekiti mteule wa Halmashauri ya Moshi kupitia chama cha mapinduzi na wa kamati ya siasa Wilaya."


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...