Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Baraza Dogo la Wafanyakazi wa wizara hiyo (hawapo pichani), wakati akifungua mkutano huo uliofanyika jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Baraza Dogo la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Kayuni akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Baraza Dogo la Wafanyakazi wa wizara hiyo (hawapo pichani), kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Christopher Kadio na kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Francis Lubeti  mkutano huo umefanyika jijini Dodoma.

Mjumbe wa Baraza Dogo la Wafanyazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kamishna wa Polisi, Albert Nyamhanga akizungumza wakati wa kikao cha baraza hilo kilichofanyika jijini Dodoma.

Mjumbe wa Baraza Dogo la Wafanyazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Abas Malekela akizungumza wakati wa kikao cha baraza hilo kilichofanyika jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

………………………………………………………………………………….

Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, amewaagiza wafanyakazi wa Wizara hiyo kutatua kwa wakati changamoto za wananchi wanaofika kutoka sehemu mbalimbali kuja kupata huduma wizarani.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kufungua Mkutano wa Baraza Dogo la Wafanyakazi wa wizara hiyo, Katibu Mkuu Kadio amewataka wajumbe wa mkutano huo kwenda kufanya kazi kwa weledi ili kuwasaidia wananchi katika kutoa huduma iliyo bora.

Alisema wananchi wanapopeleka changamoto zao ni wajibu wao kuzitatua na kuwarudishia kwa wakati kwa sababu ni wajibu wao kufanya kazi hizo.

“Nyie wajumbe wa Baraza mkawe mfano wa kuigwa katika vitengo vyenu vya kazi, masuala mliyojadili katika mkutano wa Baraza mkawape elimu wenzenu waliowachagua kuwawakilisha” alisema Kadio

Kadio pia   aliwapongeza viongozi waliochaguliwa katika Baraza hilo na kuwataka kwenda kuwa mfano bora katika maeneo yao ya kazi.

Alisema watumishi wenzenu wana Imani kubwa na nyie hivyo nanyi mkafanye kazi ya kutathmini mtumishi mmoja mmoja ili kuboresha mazingira yao ya kazi kwa ujumla.

Alifafanua zaidi mkajenge utaratibu wa kukutana na menejimenti ya wizara ili kushauri namna ya kuweka mikakati bora ya ufanyaji kazi kwa watumishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...