Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Waziri
Kindamba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isuli katika uzinduzi wa mnara
wa mawasiliano wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora.
Wananchi wa kijiji cha Isuli, wilayani Uyui mkoa
wa Tabora walijitokeza kwa wingi katika
uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano kijijini hapo.
Wananchi wa kijiji cha Isuli wakifanya usajili
wa laini za simu za TTCL Corporation katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa
mawasiliano uliofanyika katiko kijiji hicho, wilayani Uyui mkoa wa Tabora.
Mbunge wa Jimbo la Igalula Venant
Daudi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isuli katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa
mawasiliano kijijini hapo.
Mkuu wa
Wilaya ya Uyui Gift Msuya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Tabora akihutubia
wakazi wa kijiji cha Isuli katika uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wilayani
Uyui, Mkoa wa Tabora.
Mkuu wa
Wilaya ya Uyui Gift Msuya, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Waziri
Kindamba, Mbunge wa Jimbo la Igalula Mhe. Mhe. Venant Daudi, Diwani
wa Kata ya Kizengi Mhe. Magidinga Masaga
na viongozi wa serikali ya kijiji wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa
mawasiliano katika kijiji cha Isuli, wilayani Uyui, mkoa wa Tabora.
1. Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Waziri
Kindamba akitoa maelezo kwa Mgeni Rasmi na Mkuu Wilaya ya Uyui Gift Msuya kuhusu mitambo ya mawasiliano iliyofungwa
katika kijiji hicho kwenye uzunduzi wa Mnara wa mawasiliano, kijijini Isuli,
wilayani Uyui, mkoa wa Tabora.
1 Diwani wa Kata ya
Kizengi Mhe. Magidinga Masaga akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Isuli katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa
mawasiliano kijijini hapo.
MKUU wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa
Tabora amezindua mnara wa mawasiliano katika kata ya Kizengi, kijiji cha Isuli wilayani
Uyui na kuwataka wananchi kutumia mawasiliano kwa ajili ya kulinda usalama na
kukuza maendeleo ya Taifa letu.
Akizindua mnara huo, Gift Msuya amesema mawasiliano ni
muhimu sana katika kulinda usalama na kukuza uchumi wa Taifa letu.
“Nawasihi wananchi wa
Isuli kutumia mawasiliano kwa ajili ya kukuza uchumi wa Taifa letu kwa kuwekeza
zaidi katika kutafuta masoko na fursa mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya
Tanzania.” amesema Mkuu wa Wilaya huyo.
Amesema wakazi wa kijiji
cha Isuli wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo vya Usalama ili sheria ichukue
mkondo wake kwa wote watakaohujumu miundombinu ya mawasiliano. Pia amesitiza kuwa
wananchi wasikubali kuona watu wachache wenye malengo yao binafsi wanaharibu
uwekezaji kama huu ambao Serikali imewekeza kwa nguvu nyingi ya kuwapatia
wananchi mawasiliano.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ameipongeza Shirika kwa kufanikisha
kupeleka mawasiliano ya simu kwenye vijiji
vya Alex- Uyui, Buhekela- Igunga, Nsenda Mlimani-Urambo, Isuli-
Uyui, Shilla- Nzega, Nsogoro-Urambo, Usunga- Sikonge, Malagano -Igunga na
vijiji vingine vya Ngulu Mpakani-Igunga, Igoweko-Uyui, Nyaua-Uyui na
Magua-Sikonge ambapo ujenzi wa minara unaendelea.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba amewataka wananchi wa kijiji
cha Isuli kuhakikisha miundombinu ya mnara huo wa
mawasiliano na miundombinu mingine ya Shirika la Mawasiliano Tanzania,
inalindwa dhidi ya wahalifu.
“ni jukumu letu
sote, tushirikiane kwa pamoja, uongozi wa Kata, wananchi pamoja na Kamati ya ulinzi
na usalama katika kulinda miundombinu hii ya mawasiliano.” amesema Mkurugenzi
Mkuu.
Aidha, Kindamba
ametoa rai kwa wananchi kutumia
huduma za vifurushi ambavyo ni vya
gharama nafuu, pia kuwataka wananchi kuchangamkia
fursa za kujiongezea kipato kwa kuwa mawakala wa kuuza vocha na mawakala wa
T-PESA.
Hata hivyo,
Mkurugenzi Mkuu amesema kuwa Shirika litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza mikakati na mipango mbalimbali ya kupeleka huduma za
mawasiliano maeneo ambayo bado yana changamoto ya mawasiliano hasa maeneo ya
vijijini na pembezoni mwa mipaka ya nchi yetu.
Akizungumza na
wananchi katika tukio hilo, Mbunge wa Jimbo la Igalula, Venant Daudi ameishukuru
Shirika la Mawasiliano Tanzania kwa kupeleka huduma ya mawasiliano katika kijiji cha Isuli,na kusema uwepo wa
mawasiliano katika kiijiji kutaondoa kero ya wananchi ya muda mrefu ya kukosa
huduma za mawasiliano.
Aidha, Mbunge huyo ametumia fursa hiyo kumuomba Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Mawasiliano kumsaidia kutatua changamoto za mawasiliano
kwenye vijiji vingine ambavyo havina huduma za mawasiliano katika jimbo la Igalula Wilayani Uyui, Tabora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...